MSD Yakabidhi Vifaa Tiba vya Mil. 500 - Hospitali ya Wilaya Kisemvule
SERIKALI kupitia Bohari ya Dawa (MSD), imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 500 kwa hospitali ya Wilaya ya Ilala (Kivule), lengo ni kuboresha hali ya utoaji huduma wilayani humo.
Vifaa hivyo ni pamoja na Vitanda vya kulalia wagonjwa, ventileta za ICU, viti mwendo, friji za kuhifadhia damu na sampuli, vitanda vya uchunguzi, Sunction machine, Ultra Sound machine, magodoro na mashuka.