MSD Kilimanjaro Yajadili Mbinu Kuboresha Uhusiano na Huduma kwa Wateja
ARUSHA.
MSD Kanda ya Kilimanjaro imekutana na wateja wake wanaopata huduma kutoka Kanda hiyo ambao ni kutoka mikoa yaArusha, Kilimanjaro na Manyara, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanagusa pande hizo, kwa lengo la kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
Mkutano huo wa siku moja umefanyika Mkoani Arusha ukiwa na lengo la kujenga uhusiano mzuri baina ya MSD Kanda ya Kilimanjaro na wateja wake wote wanaohudumiwa na Kanda hiyo.