Wateja wa MSD Kanda ya Tanga Wapongeza Maboresho ya Huduma za MSD
Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga wameipongeza MSD kwa maboresho makubwa inayoendelea kuyafanya ya usambazaji wa bidhaa za afya kwa wakati.
Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD ambaye pia ni Mlezi wa MSD kanda hiyo, Dkt. Rukia Mwifunyi anayoifanya mkoani humo, kuzungumza na wateja wanaowahudumia ili kupata maoni yao juu ya huduma za MSD na kupokea changamoto zao ili ziweze kufanyiwa kazi.