Skip to main content

MAFANIKIO YA MSD KATIOKA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

UPATIKANAJI WA BIDHAA ZA AFYA

Bohari ya Dawa imeendelea kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya. Uwepo wa bidhaa za afya umekuwa ukipimwa kwa bidhaa za afya ashiria 290 lakini kutokana na kuimarishwa mifumo ya utoaji huduma na nia ya Serikali kuboresha maisha ya Watanzania kuanzia mwaka wa fedha 2023/24, idadi ya bidhaa ashiria zinazotumika kupima hali ya upimaji wa bidhaa za afya zimeongezeka kutoka bidhaa 290 hadi kufikia bidhaa 382.

Hali ya uwepo wa bidhaa za afya ashiria 382 imeongezeka kutoka asilimia 42 mwaka 2021/2022 hadi asilimia 67 mwezi Februari, 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 23. Kwa ujuma hali ya upatikani wa bidhaa za afya umekuwa ukiimarika mwaka hadi mwaka.

 

UTIMIZAJI WA MAHITAJI YA BIDHAA ZA AFYA

Hali ya utimizaji wa mahitaji ya vituo vya kutolea huduma za afya umeendelea kuimarika ambapo hadi mwezi Juni 2024, hali ya utimizaji wa mahitaji ulifikia asilimia 79. Hata hivyo kutokana na uwepo wa migororo mbalimbali inayoendelea duniani na hivyo kuathiri mnyororo wa ugavi pamoja na uzalishaji wa viwanda nchini usiondena na ongezeko la mahitaji ya vituo vya kutolea huduma za afya, hali ya utimizaji wa mahitaji umefikia asilimia 67 na unatarajia kufika asilimia 90 ifikapo mwezi Juni 2025. Ongezeko hili linatokana na kuimarishwa kwa mkakati wa kununua bidhaa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji

 

MPANGO MAALUM WA USAMBAZAJI WA MASHINE ZA UCHUJAJI DAMU “ DIALYSIS”.

Serikali kupitia Bohari ya Dawa inatekeleza mpango maalumu wa kuongeza upatikanaji wa huduma za uchujaji wa damu ikiwa ni sehemu ya matibabu ya figo, hivyo kupunguza gharama za huduma hiyo. Kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ya awamu ya sita, hadi kufikia mwezi Februari 2025, idadi ya mashine imeongezeka na kufikia mashine 137 kutoka mashine 60 na hivyo kuongeza idadi ya hospitali zilizopokea mashine kutoka Bohari ya Dawa kutoka hospitali 6 zilizokuwepo mwaka wa fedha 2021/22 na kufikia hospitali 15 mwaka 2024/25. Uwekezaji huu uliofanyika umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 7.7.

Katika hospitali hizi, hospitali 11 zimeanza kutoa huduma na hospitali 4 zipo katika hatua ya matengenezo. Baadhi ya hospitali zinazotoa huduma ni pamoja na Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Amana, Mwananyamala ,Temeke, Morogoro, Katavi, Tumbi, Chato, Sekoe Toure na UDOM Hospitali.

 

USAMBAZAJI WA BIDHAA ZA AFYA ZA KINYWA.

Usambazaji wa bidhaa za afya ya kinywa na meno umeendelea kuimarika katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita ambapo Bohari ya Dawa imeendelea kuhakikisha bidhaa za afya ya kinywa na meno zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya. Aidha, kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali kupitia Bohari ya dawa imesambaza bidhaa za afya za kinywa na meno zenye thamani ya shilingi bilioni 9.98 kutoka kusambaza bidhaa za afya za kinywa na meno zenye thamani ya shilingi milioni 254.7 kwa mwaka 2021/2022. Katika kipindi cha miaka minne mfululizo bidhaa za afya za kinywa na meno zenye thamani ya shilingi bilioni 21.5 zimesambazwa, ambapo shilingi bilioni 17.87 ni thamani ya viti vya kutolea huduma za kinywa na meno na pamoja na mashine za mionzi ya kinywa na meno ambayo ni sawa na asilimia 83. Katika gharama hii, viti vya huduma za kinywa na meno vimegharimu shiling bilioni 13.8 na kuwezesha kusambazwa kwa viti 647 na mashine za kisasa za mionzi za kinywa na meno zikiwa ni 331 zenye thamani ya shilingi bilioni 4.07.

 

USAMBAZAJI WA BIDHAA ZA MAMA NA MTOTO (CEMONC).

Katika kuboresha afya ya mama na mtoto kwa kutoa huduma za dharura za uzazi pingamizi na huduma za awali kwa watoto wachanga, Serikali kupitia Bohari ya Dawa katika kipindi cha miaka minne imenunua na kusambaza bidhaa za afya, kwa ajili ya kuboresha vituo vya afya 316 na kuhakikisha vinatoa huduma ya dharura ya uzazi na mtoto - Comprehensive Emergency Obstetric and New-born Care - CEmONC. Bidhaa zote za afya 414 zenye thamani ya shilingi 100,182,390,897.40 zimekwisha sambazwa na kusimikwa kwenye vituo hivyo vya kutolea huduma za afya nchini.

MAPITIO YA MFUMO WA TEHAMA

Kwa ujumla Matumizi ya TEHAMA kwa Bohari ya Dawa yamefikia asilimia 95 ambapo sehemu kubwa ya michakato inafanyika katika mfumo wa Epicor 10 – ERP na kupelekea MSD kutambulika na Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa kiwango cha Level 4 katika 11

matumizi ya Tehama. Aidha, Bohari ya Dawa imeendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali kuhusu mifumo ya TEHAMA kusomana ambapo mifumo iliyounganishwa ni pamoja na (ELMIS) ambao hutumika kupokea mahitaji kutoka vituo vya kutolea huduma za afya, HFR-kupata taarifa za usajili wa kituo cha kutolea huduma za afya, Mifumo ya malipo (Benki na GePG), DCEA- taarifa za ununuzi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizothibitishwa, Epicor-taarifa ya fedha zilizotolewa na wafadhili na malipo yaliyotumika, NHIF-kusaidia kupata taarifa ya bei (kitita cha NHIF), Mfumo wa TMDA- Kupata taarifa ya bidhaa zilizosajiliwa na GoTHOMIS-taarifa ya bei za bidhaa, maombi ya wateja, orodh a ya wateja n.k,

 

KUBORESHA MNYORORO WA UGAVI

Bohari ya Dawa ilikusudia kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za afya unaimarika, bidhaa za afya zinafika kwa wananchi kwa wakati na mabadiliko yanayotokea kwenye vituo vya kutolea huduma za afya yanafahamika MSD na hatua muhimu kuchukuliwa ili kuepusha ukosefu wa bidhaa za afya. Aidha, Bohari ya Dawa ilitambua umuhimu wa kujipanga na kuweza kukabiliana na majanga mbalimbali pindi yanapotokea na kuimarisha mifumo ili kuhakikisha bidhaa zinazopokelewa zinaendana na zile zilizoagizwa

 

UTEKELEZAJI WA SERA YA VIWANDA

MSD imekuwa katika jitihada za kuanzisha viwanda vyake yenyewe kupitia mfumo wa Public Private Partnership (PPP) kwa mujibu wa Sheria ya PPP kwa kipindi kirefu lakini hatukufanikiwa kutokana na kukinzana kwa taratibu, masharti na namna ya utekelezaji wa mradi kwa mujibu wa sheria za PPP ikiwemo muda mrefu wa mradi na MSD kukosa umiliki katika uwekezaji. Hata hivyo, Mwaka 2021, Serikali ilifanya marekebisho ya Sheria ya Bohari ya Dawa na kuongeza rasmi jukumu la Uzalishaji Dawa na Vifaa tiba kwa MSD. Katika kutekeleza jukumu hili MSD ilifanya mageuzi makubwa ya kiusimamizi kwa kuanzisha Kampuni Tanzu “MSD Medipharm Manufacturing Co.LTD” ambayo inasimamia viwanda na jukumu la uzalishaji kwa asilimia 100 na ina mamlaka kisheria kuingia makubaliano ya ushirikiano na Kampuni mbalimbali za uwekezaji na kuwekeza pamoja.

 

KUONGEZA UNUNUZI WA BIDHAA ZA AFYA KUTOKA KWA WAZALISHAJI WA NDANI

Serikali kupitia Bohari ya Dawa imeendelea kuongeza ununuzi wa bidhaa za afya kutoka kwa wazalishaji wa ndani ambapo kwa kipindi cha Julai-Disemba 2024/2025, bidhaa za afya zenye thamani ya shilingi bilioni 56.7 zimenunuliwa kutoka shilingi bilioni 22.1 zilizonunuliwa mwaka 2023/24 ikiwa ni ongezeko la asilimia 157. Dhamira hii itasaidia kuongeza uzalishaji na kuvutia wawekezaji ambapo matumizi ya fedha za kigeni yatapungua na ajira zitatengenezwa nchini.

 

UJENZI WA MAGHALA YA KUHIFADHI BIDHAA ZA AFYA

Kwa kutambua ongezeko la mahitaji na muelekeo wa kuwekeza kwenye nishati mbadala, Serikali kupitia Bohari ya Dawa imeanza ujenzi wa maghala mapya toka mwezi Agosti 2023 katika Kanda ya Mtwara na Dodoma ili kukidhi upungufu uliojitokeza. Ujenzi huu unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Machi 2025 na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 42. Fedha zinazotumika katika ujenzi wa maghala zimetolewa na Serikali.

 

UJENZI WA MAGHALA YA KUHIFADHI BIDHAA ZA AFYA

Kwa kutambua ongezeko la mahitaji na muelekeo wa kuwekeza kwenye nishati mbadala, Serikali kupitia Bohari ya Dawa imeanza ujenzi wa maghala mapya toka mwezi Agosti 2023 katika Kanda ya Mtwara na Dodoma ili kukidhi upungufu uliojitokeza. Ujenzi huu unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Machi 2025 na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 42. Fedha zinazotumika katika ujenzi wa maghala zimetolewa na Serikali.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.