MSD YAKABIDHI JENERETA LA KVA 75 KWA HOSPITALI YA WILAYA YA KITETO
Hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara imeondokana na changamoto ya kukatiza baadhi ya huduma za matibabu kama upasuaji na pindi umeme unapokatika baada ya Bohari kuu ya dawa MSD kukabidhi jenereta lenye thamani ya shilingi milioni 65 itakayotumika kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano mjini Kibaya wilayani Kiteto, meneja wa MSD kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa amesema jenereta hilo lenye uwezo wa KVA 75 ni sehemu ya mahitaji ya vifaa vya afya vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 699 vilivyoagizwa na hospitali hi