Bohari ya Dawa (MSD) Kukuza Ushirikiano na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
Bohari ya Dawa (MSD) imekutana ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) lengo likiwa kuanzisha ushrikiano wa kiutendaji kwenye nyanja za Utafiti, Ubunifu, Teknolojia, TEHAMA, Biashara na Fedha. Kikao hiko cha ushirikiano kimefanyika Makao Makuu ya MSD Keko Dar es Salaam, huku kikikutanisha maafisa mbalimbali kutoka kwenye taasisi hizo.
Akizungumza kwenye kikao hicho Kaimu Rasi Ndaki ya Sayansi za Komputa na Elimu Angavu Dkt. Florence Rashid amesema ushirikiano huu utakwenda kuifaidisha MSD kwa kuwa UDOM ina wataalamu waliobobea kwenye nyanja za Utafiti, Ubunifu, Teknolojia, TEHAMA, Biashara na Fedha ambapo wataalamu hao watakwenda kuchagiza makubaliano yaliyofikiwa kwenye kikao hiki.
“Pamoja na mambo mengi tuliyokubaliana, maeneo makubwa ambayo MSD kwa sasa ni moja ya vipaumbele vyake ni pamoja na TEHAMA na Tekinolojia. Chuo Kikuu cha Dodoma tumewaakikishia MSD kuwapa ushirikiano mzuri ili waendelea kutoa huduma nzuri kwa wananchi. Aliongeza Dkt. Rashid.
Kwa upande wake Kamu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Ndg. Hans Mwambuba amesema kuwa MSD imekiomba Chuo Kikuu cha Dodoma kuendelea kuratibu utoaji wa elimu bora kwa wahitimu wake hasa wa Ugavi kwani ndio wanaokuja kufanya kazi kwenye sehemu kubwa ya MSD.
“ Tumekiomba Chuo Kikuu cha Dodoma kuharakisha ukamilishwaji wa Shule ya Uandisi vifaa tiba kwani ni sehemu ambayo MSD na nchi kwa ujumla inauhitaji mkubwa wa wataalamu hao kwenye maeneo hayo. Aliongeza Ndg. Mwambuba
- Log in to post comments