Skip to main content

Wizara ya Afya Somalia, Yaja Kujifunza MSD na Kubadilishana Uzoefu

Wizara ya Afya nchini Somalia imeichagua  Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kushirikiana kwenye masuala mbalimbali yanayohusu mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya kwa  kubadilishana uzoefu katika maeneo ya mifumo, ununuzi, usambazaji na udhibiti ubora.

Hayo yamebainishwa na watendaji wa Wizara ya Afya kutoka nchini Somalia waliotembelea Bohari ya Dawa (MSD), ambapo mwakilishi wa ugeni huo Mohamed Abdulukadiri Hersi  ameeleza kuwa  hatua mbalimbali zilizofanywa na Serikali ya  Tanzania kupitia Bohari ya Dawa katika mifumo inayotumika katika mnyororo mzima wa ugavi inayotumia tekinolojia ndio umewavutia zaidi kuja kujifunza kwa kujionea namna inavyofanya kazi na kuoana na mifumo mingine ya serikali.

Hersi  ameongeza kuwa, Somalia ipo kwenye mpango wa kujenga upya mfumo wake wa ugavi wa bidhaa za afya, ikiwa ni pamoja na kuboresha utaratibu wa kufikisha bidhaa za afya kwa wananchi, hivyo kati ya nchi walizozichagua kuwa mfano ni Tanzania, ambapo kupitia MSD amesema wamemejifunza mengi ambayo watakwenda kuyatekeleza watakaporudi. 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai, ameeleza kuwa wageni hawa wamekuja Tanzania kwa muda muafaka ambapo MSD imefanya mageuzi makubwa ya kiutendaji ikiwemo kujiendesha kibiashara, na kufanya maboresho mbalimbali katika mnyororo mzima wa ugavi wa bidhaa za afya, hivyo watajifunza mengi.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.