Skip to main content

MSD Yapongezwa kwa Mabadiliko na Maboresho ya Kiutendaji Katika Kipindi cha Miaka 30

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert Ndaki ameipongeza Bohari ya Dawa(MSD) kwa kuboresha huduma kwa wateja, sambamba na upatikanaji wa bidhaa za afya kwa wakati, hali iliyowezesha kupungua kwa malalaiko ya wateja na wananchi kwa ujumla.

Dkt. Ndaki ametoa pongezi hizo hii leo tarehe 21/11/2024 mbele ya Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Bw. Ally Seleman wakati ujumbe kutoka MSD ulipotembelea kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza mbele ya ujumbe wa MSD, Dkt. Ndaki ameipongeza MSD kwa kutimiza miaka thelathini (30) ya utendaji, huku akibainisha maboresho ya huduma zake na jinsi yalivyosaidia katika upatikanaji wa bidhaa za afya.

Dkt. Ndaki amebainisha kuwa mabadiliko ya mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya kutoka miezi minne (4) hadi sita (6) kwa mwaka, yameleta ahueni kwa wananchi kwani hivi sasa upatikanaji wa bidhaa za afya vituoni ni wa kuridhisha, ambapo hivi sasa upatikanaji umepanda hadi kufikia asilimia 75 hadi 80, ukilinganisha na chini ya asilimia 50 ya miaka ya nyuma.

Katika hatua nyingine, Dkt. Ndaki ameeleza jinsi maboresho ya Uhusiano na huduma kwa wateja, (customer service) baina ya MSD na Wateja wake, yalivyosaidia katika kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Bw. Ally Seleman amesisitiza kwamba MSD itaendelea kushirikiana kwa ukaribu na wateja wake, sambamba na kufanyia kazi maoni yote yanayotolewa na wateja kwa lengo la kuboresha utendaji na kuleta tija kwa jamii.

Ameongeza kuwa, MSD inaendelea na mchakato wa mabadiliko ya ndani kiutendaji Ili kuhakikisha inakidhi matakwa ya wateja wake, na kuongeza ufanisi na tija katika kuhudumia wananchi.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.