Somalia Kushirikiana na MSD, Ununuzi wa Bidhaa za Afya
Rais wa Somalia Mheshimiwa Hassan Sheikh Mohamud amesema nchi yake imeamua kushirikiana kwa karibu na Bohari ya Dawa ya Tanzania katika ununuzi wa bidhaa za afya na kubadilishana uzoefu wa namna mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya unavyofanya kazi.
Rais Mahamud ambaye yuko ziarani nchini Tanzania, ameyasema hayo alipoitembelea MSD, na kuongeza kuwa kutokana na uzoefu wa MSD, wana uhakika kuwa ubora wa bidhaa za afya utakuwa wa uhakika.