Wadau na wateja wa MSD wamekumbushwa kuendelea kushirikiana
Wadau na wateja wa MSD wamekumbushwa kuendelea kushirikiana kwa karibu ili kihakikisha wanaendelea kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya nchini na kuwa utaratibu wa kulipa madeni ili kuiwezesha MSD kuwa na mtaji mzuri wa kuendelea kununua bidhaa za afya.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt.Charles Rashid Mkombachepa alipokuwa anafungua kikao cha mwaka cha wadau na wateja wa MSD kanda ya Kilimanjaro wa mkoani wa Arusha. Dkt. Mkombachepa amewakumbusha watendaji hao kuwa ubora wa huduma za MSD tunazoziona leo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya umechangiwa na upatikanaji mzuri wa fedha za kuiendesha MSD.
Hata hivyo Dkt. Mkombachepa ameipongeza MSD kwa kuboresha huduma kwa mkoa wa Arusha ambapo huduma hizo zilizoboreshwa zimewezesha kuongezeka kwa upatikanaji wa bidhaa za afya hadi kufikia zaidi ya asilimia 90%.
Dkt.Mkombachepa amesema kutokana na maboresho hayo ambayo MSD inayafanya, malalamiko yamepungua, lakini amesisitiza kuwa ni vizuri tukakaa pamoja na kutatua changamoto chache zilizobakia ili kuzungumzia maboresho zaidi kuliko malalamiko.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha wa MSD Undule Koroso amesema vikao hivi vina umuhimu kwa MSD kwani vinaboresha mahusiano na mawasiliano kati ya MSD na wataja wake na wateja wanapata wasaa wa kukutana ana kwa ana na MSD kuzungumza masuala ya kuboresha katika mnyororo mzima wa bidhaa za afya.
- Log in to post comments