Skip to main content
 • Serikali Yamwaga Vifaa Tiba vya Milioni 222.472 Mkoani Singida

  SERIKALI  ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi vifaa tiba Mkoa wa Singida vyenye jumla ya takribani Sh.Milioni 222.472, kwaajili ya kuboresha huduma za afya Mkoani humo.

  Vifaa hivyo ni pamoja na majenereta, sambamba na vifaa vitakavyotumika kuhudumia watoto wanaozaliwa kabla ya muda na huduma nyinginezo ambavyo vimekabidhiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Ikungi, Kituo cha Afya Sepuka na Hospitali ya Wilaya ya Singida, Ilongero.

 • Uongozi wa Juu USAID na PEPFAR Watembelea MSD Kanda ya Iringa

  Mkurugenzi Mkazi wa USAID Tanzania Craing Hart na Mratibu Mkuu wa PEPFAR Tanzania Jessica Greene wametembelea MSD Kanda ya Iringa kuangalia namna MSD inavyotekeleza Majukumu yake, hasa ununuzi, utunzaji, na usambazaji wa bidhaa za afya zinazofadhiliwa na Mifuko hiyo.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara hiyo, Bw. Hart na Bi. Greene wameipongeza MSD kwa weledi wake katika usimamizi na usambazaji wa bidhaa za miradi misonge hadi kwa walengwa ambao ni wananchi.

 • MSD Yateta na Wazalishaji wa Ndani wa Bidhaa za Afya.

  #DAR ES SALAAM

  Wazalishaji wa ndani wa bidhaa za afya wamehakikishiwa soko la ndani na nje la bidhaa wanazozalisha, huku wakisisitizwa kuzingatia kiasi cha mahitaji na ubora wa bidhaa hizo.

  Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa Wazalishaji wa ndani wa bidhaa za afya ulioandaliwa na Bohari ya Dawa (MSD) Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi amesema kuwa serikali ina dhamira ya kuwawezesha wazalishaji wa ndani hasa katika masuala ya sheria na taratibu zinazohusiana na viwanda vya bidhaa za afya.

 • Serikali Yakabidhi Vifaa Tiba vya Milioni 900 Halmashauri ya Ifakara

  #MOROGORO

  SERIKALI kupitia Bohari ya Dawa (MSD), imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya sh milioni 900 kwa Halmashauri ya Ifakara mji.

  Akizungumza jana Mkoani humo, Mbunge wa Kilombero Mhe.Abubakar Asenga, alisema ujio wa vifaa hivyo, utasaidia kuboresha huduma za afya hivyo wanaishukuru serikali kwa hatua kubwa ya maboresho katika sekta hiyo.

 • Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Aonya Matumizi Mabaya ya Vyandarua

  #SONGWE

  MKUU wa Mkoa wa Songwe, Dk. Francis Michael, ameonya matumizi mabaya ya vyandarua kama vile kufugia kuku au kuvulia samaki.

  Akizungumza jana mkoani humo wakati akizinduza mpango wa ugawaji wa vyandarua katika shule za msingi Dk.Micheal amesisitiza kuwa vitendo hivyo vinaathiri juhudi za Serikali na wadau wa afya katika kupambana na Malaria.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.