Skip to main content

MSD YASHINDA TUZO TATU ZA MWAJIRI BORA 2024

Bohari ya Dawa (MSD) imejinyakulia tuzo tatu za Mwajiri bora mwaka 2024 kupitia tuzo zinazotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

Katika tuzo hizo zilizotolewa na Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dotto Biteko, MSD imeibuka na ushindi wa tuzo tatu ambazo ni pamoja na Taasisi bora kiutendaji (Club of Ten best performers), mshindi wa kwanza kwa taasisi inayotoa fursa za ajira (First runner up job creation na mshindi wa pili Mwajiri bora sekta ya umma (Second runner up Public Sector).

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hizo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu MSD Mboyi Wishega, ameeleza kwamba MSD imefanikiwa kupata tuzo hizo kwa sababu ya uongozi wa thabiti wa Mkurugenzi Mkuu, Bw. Mavere Tukai, katika kusimamia utekelezaji wa mabadiliko ya utendaji ndani ya MSD, ili kuhakikisha malengo yote ya kuanzishwa kwake na yale ya Mpango Mkakati yanafikiwa.

Ameongeza kuwa siri nyingine ya ushindi ni ushirikiano mzuri kati ya Menejimenti na watumishi wote wa MSD katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku. Amebainisha kwamba Utamaduni huo wa kushirikiana, ni tunu muhimu iliyopelekea ushindi wa tuzo hizo.

Wishega ametoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita, Chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Afya kwa ujumla, kwa ushirikiano mzuri ambao wamekuwa wakiipatia MSD, kwani umekuwa chachu ya kuiwezesha MSD kutimiza majukumu yake kwa ufanisi

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.