MSD Yaanza Usambazaji wa Vifaa Tiba kwa Majimbo ya Mkoa wa Morogoro
BOHARI ya Dawa (MSD) imeanza usambazaji majimboni vifaa tiba vilivyonunuliwa na serikali vyenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 14.9 kwa ajili ya hospitali, vituo vya afya na zahanati lengo ni kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Meneja wa MSD, Kanda ya Dar es salaam, inayohudumia mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Visiwa vya Zanzibar, Betia Kaema alisema hayo wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , Adam Malima kwa ajili ya majimbo 11 ya Mkoa huo.