MSD Kuimarisha Upatikanaji wa Bidhaa za Maabara Nchini.
Bohari ya Dawa (MSD) imeadhimia kuboresha hali ya upatikanaji wa bidhaa za maabara nchini, ili kuimarisha uchunguzi wa vimelea vya magonjwa mbalimbali nchini.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya (MSD) Rosemary Silaa, wakati alipotembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa - Bukoba na hospitali ya Wilaya ya Bukoba vijijini, ziara iliyolenga kupokea mrejesho wa huduma za MSD kutoka kwa wateja, ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 30 toka MSD kuanza kazi zake rasmi.