Rais Samia Atoa Vifaa Tiba vya Mil. 691 Kwa Majimbo 10 - Dar es Salaam
RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan ameendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya hususani huduma ya mama na mtoto lengo likiwa ni kupunguza vifo vitonavyo na uzazi pingamizi.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila alipokuwa akiwakabidhi wabunge wa majimbo 10 ya mkoa wa Dar es Salaam, vifaa tiba vyenye thamani ya sh. Milioni 691 vilovyotolewa na serikali kwa majimbo hayo.