Aller au contenu principal

MAFANIKIO YA MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA

UPATIKANAJI WA BIDHAA ZA AFYA

Bohari ya Dawa imeendelea kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya. Uwepo wa bidhaa za afya umekuwa ukipimwa kwa bidhaa za afya ashiria 290 lakini kutokana na kuimarishwa mifumo ya utoaji huduma na nia ya Serikali kuboresha maisha ya Watanzania kuanzia mwaka wa fedha 2023/24, idadi ya bidhaa ashiria zinazotumika kupima hali ya upimaji wa bidhaa za afya zimeongezeka kutoka bidhaa 290 hadi kufikia bidhaa 382.  Hali ya uwepo wa bidhaa za afya ashiria 382 imeongezeka kutoka asilimia 42 mwaka 2021/2022 hadi asilimia 67 mwezi Februari, 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 23. Kwa ujuma hali ya upatikani wa bidhaa za afya umekuwa ukiimarika mwaka hadi mwaka.

Aidha, kwa kipindi hicho cha miaka minne, Bohari ya Dawa imefanya ununuzi na usambazaji wa vifaa na vifaa tiba vinavyohitajika katika vituo vya kutolea huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi vituo vinavyotoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi nchini. Vifaa vingi katika hivi hutumika kufanya uchunguzi na kuwezesha vituo vya kutolea za afya kutimiza majukumu yao ipasavyo. Baadhi ya vifaa vilivyosambazwa ni pamoja na mashine za usingizi, CT- Scan, MRI 3T, Ultrasound mashine, na digital X-Ray vyenye jumla ya shilingi bilioni 376.6

UTIMIZAJI WA MAHITAJI YA BIDHAA ZA AFYA

Hali ya utimizaji wa mahitaji ya vituo vya kutolea huduma za afya umeendelea kuimarika ambapo hadi mwezi Juni 2024, hali ya utimizaji wa mahitaji ulifikia asilimia 79. Hata hivyo kutokana na uwepo wa migororo mbalimbali inayoendelea duniani na hivyo kuathiri mnyororo wa ugavi pamoja na uzalishaji wa viwanda nchini usiondena na ongezeko la mahitaji ya vituo vya kutolea huduma za afya, hali ya utimizaji wa mahitaji umefikia asilimia 67 na unatarajia kufika asilimia 90 ifikapo mwezi Juni 2025. Ongezeko hili linatokana na kuimarishwa kwa mkakati wa kununua bidhaa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji.

MPANGO MAALUM WA USAMBAZAJI WA MASHINE ZA UCHUJAJI DAMU

Serikali kupitia Bohari ya Dawa inatekeleza mpango maalumu wa kuongeza upatikanaji wa huduma za uchujaji wa damu ikiwa ni sehemu ya matibabu ya figo, hivyo kupunguza gharama za huduma hiyo. Kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ya awamu ya sita, hadi kufikia mwezi Februari 2025, idadi ya mashine imeongezeka na kufikia mashine 137 kutoka mashine 60 na hivyo kuongeza idadi ya hospitali zilizopokea mashine kutoka Bohari ya Dawa kutoka hospitali 6 zilizokuwepo mwaka wa fedha 2021/22 na kufikia hospitali 15 mwaka 2024/25. Uwekezaji huu uliofanyika umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 7.7.

Katika hospitali hizi, hospitali 11 zimeanza kutoa huduma na hospitali 4 zipo katika hatua ya matengenezo. Baadhi ya hospitali zinazotoa huduma ni pamoja na Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Amana, Mwananyamala ,Temeke, Morogoro, Katavi, Tumbi, Chato, Sekoe Toure na UDOM Hospitali.

Mkakati huu wa usambazaji wa mashine za dialysis unalenga kupunguza gharama ambapo kwa sasa gharama zinazotozwa ni kati ya shilingi 200,000 na shilingi 230,000 na matarajio ni kuweza kupunguza na kuwa chini ya shilingi 100,000 kwa ‘session’ moja. Mkakati huu unatekelezwa chini ya uratibu imara wa Wizara ya Afya kwa kushirkiana na hospitali zinazotoa huduma za hemodialysis ambapo kifurushi cha msingi cha vifaa vinavyotumika katika hemodialysis kwa ajili ya vipindi 100. (hemodialysis consumables basic kit content for 100 sessions) kimeanzishwa. Kifurushi hiki kina jumla ya bidhaa muhimu 15 kwa kila kipindi kimoja cha dialysis.

USAMBAZAJI WA BIDHAA ZA AFYA ZA KINYWA.

Usambazaji wa bidhaa za afya ya kinywa na meno umeendelea kuimarika katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita ambapo Bohari ya Dawa imeendelea kuhakikisha bidhaa za afya ya kinywa na meno zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya. Aidha, kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali kupitia Bohari ya dawa imesambaza bidhaa za afya za kinywa na meno zenye thamani ya shilingi bilioni 9.98 kutoka kusambaza bidhaa za afya za kinywa na meno zenye thamani ya shilingi milioni 254.7 kwa mwaka 2021/2022. Katika kipindi cha miaka minne mfululizo bidhaa za afya za kinywa na meno zenye thamani ya shilingi bilioni 21.5 zimesambazwa, ambapo shilingi bilioni 17.87 ni thamani ya viti vya kutolea huduma za kinywa na meno na pamoja na mashine za mionzi ya kinywa na meno ambayo ni sawa na asilimia 83. Katika gharama hii, viti vya huduma za kinywa na meno vimegharimu shiling bilioni 13.8 na kuwezesha kusambazwa kwa viti 647 na mashine za kisasa za mionzi za kinywa na meno zikiwa ni 331 zenye thamani ya shilingi bilioni 4.07. Bidhaa hizi zimesambazwa katika hospitali 6 za ngazi ya Mkoa na Wilaya.

USAMBAZAJI WA BIDHAA ZA MAMA NA MTOTO (CEMONC).

Katika kuboresha afya ya mama na mtoto kwa kutoa huduma za dharura za uzazi pingamizi na huduma za awali kwa watoto wachanga, Serikali kupitia Bohari ya Dawa katika kipindi cha miaka minne imenunua na kusambaza bidhaa za afya, kwa ajili ya kuboresha vituo vya afya 316 na kuhakikisha vinatoa huduma ya dharura ya uzazi na mtoto - Comprehensive Emergency Obstetric and New-born Care - CEmONC. Bidhaa zote za afya 414 zenye thamani ya shilingi 100,182,390,897.40 zimekwisha sambazwa na kusimikwa kwenye vituo hivyo vya kutolea huduma za afya nchini.

UFANISI WA USAMBAZAJI WA BIDHAA ZA AFYA KWA KUZINGATIA MUDA ULIOWEKWA.

Katika kuhakikisha bidhaa za afya zinapatikana wakati wote kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, Serikali kupitia Bohari ya Dawa imeendelea kufanikisha usambazaji wa bidhaa za afya nchi nzima kwa mizunguko sita (vituo kupelekewa bidhaa kila baada ya miezi miwili) kutoka mizunguko minne (vituo kupelekewa bidhaa kila baada ya miezi mitatu) na hivyo kuhakikisha vituo vya kutolea huduma za afya zinakuwa na dawa toshelevu muda wote.

Aidha, Bohari ya Dawa imeendelea kuboresha usambazaji wa bidhaa za afya kwa wakati kwa asilimia 98 kutoka katika maghala yake hadi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Asilimia hii imeongezeka kutoka asilimia 23 iliyoripotiwa mwaka 2021/2022.

USIMAMIZI WA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU, NA MIONGOZO MBALIMBALI YA SERIKALI

Bohari ya Dawa imeendelea kufanya maboresho kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni, ikiwemo miongozo mbalimbali ya UTUMISHI, TRA, OSHA, Mifuko ya Jamii, n.k, hivyo kuwezesha kupungua kwa hoja za kikaguzi kutoka hoja 130 mwaka 2020/21 na kufikia hoja 44 mwaka wa fedha 2023/24. Ili kuondokana na hoja hizi, hatua mbalimbali zinachukuliwa ikiwemo usimikaji wa mifumo ya TEHAMA, ujenzi wa maghala, maboresho na uimarishaji wa usimamizi.

MABORESHO YA UTENDAJI WA BOHARI YA DAWA.

Mwaka 2021/22, utendaji wa Bohari ya Dawa ulikuwa ukilalamikiwa na wadau mbalimbali wa sekta ya afya kutokana na mapungufu yaliyokuwepo. Malalamiko haya yalihusu kutopatikana kwa bidhaa za afya ashiria toshelevu, uchelewaji wa kuhudumia mahitaji ya wateja ikiwemo usambazaji wa bidhaa husika, mapungufu ya mfumo wa 10  utawala bora na usimamizi wa utendaji. Wakati huu, sekta ya afya ilikuwa inakuwa kwa kasi ambapo mahitaji na aina ya bidhaa za afya yaliongezeka kutokana na kukuwa kwa Sayansi na Teknolojia na kuongezeka kwa uwekezaji uliofanywa na Serikali.

Mnamo mwezi Machi 2022, Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alitoa maelekezo ya mfumo na utendaji wa Bohari ya Dawa ufanyiwe mapitio na ufumuliwe wote ili kuendana na mahitaji sasa ya vituo vya kutolea huduma za afya na kujiendesha kwa ufanisi. Kutokana na maelekezo hayo, Bohari ya Dawa ilimtafuta mshauri muelekezi aweze kufanya mapitio na kushauri namna bora ya uendeshaji wa Taasisi.

MAPITIO YA MUUNDO WA TAASISI

Kufanya mapitio ya Muundo wa Taasisi ili kuweza kuakisi mahitaji na matarajio ya wadau mbalimbali. Eneo hili linahusisha mapitio ya ujuzi, idadi na uwezo wa watumishi kutekeleza majukumu yao.

Hatua iliyofikiwa;

i. Muundo wa Taasisi unaoakisi mahitaji umeweza kupitiwa na Mamlaka husika zimeidhinisha matumizi yake na kuweza kuakisi mahitaji ya huduma kwa wateja wakubwa, utekelezaji wa majukumu kwa kuzingatia mwenendo wa huduma za afya duniani, usimamizi wa Mradi Msonge na uimarishaji wa usambazaji wa bidhaa za afya.

ii. Watumishi wanaokidhi vigezo vya mnyororo wa bidhaa za afya wameweza kuajiriwa ikiwemo Madaktari wa Binadamu, Kinywa, Radiolojia, Wahandisi Vifaa tiba, Umeme, Wataalam wa Maabara nk.

iii. Watumishi wamepewa mafunzo yanayoendana na utendaji wa kazi zao ikiwemo mafunzo ya ununuzi, usimamizi wa Utendaji, Uendeshaji wa Taasisi nk.

MAPITIO YA MFUMO WA TEHAMA

Kwa ujumla Matumizi ya TEHAMA kwa Bohari ya Dawa yamefikia asilimia 95 ambapo sehemu kubwa ya michakato inafanyika katika mfumo wa Epicor 10 – ERP na kupelekea MSD kutambulika na Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa kiwango cha Level 4 katika 11 matumizi ya Tehama. Aidha, Bohari ya Dawa imeendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali kuhusu mifumo ya TEHAMA kusomana ambapo mifumo iliyounganishwa ni pamoja na (ELMIS) ambao hutumika kupokea mahitaji kutoka vituo vya kutolea huduma za afya, HFR-kupata taarifa za usajili wa kituo cha kutolea huduma za afya, Mifumo ya malipo (Benki na GePG), DCEA- taarifa za ununuzi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizothibitishwa, Epicor-taarifa ya fedha zilizotolewa na wafadhili na malipo yaliyotumika, NHIF-kusaidia kupata taarifa ya bei (kitita cha NHIF), Mfumo wa TMDA- Kupata taarifa ya bidhaa zilizosajiliwa na GoTHOMIS-taarifa ya bei za bidhaa, maombi ya wateja, orodh a ya wateja n.k,

Sambamba na hilo, Bohari ya Dawa imepiga hatua kubwa katika mpango wake wa kudijiti michakato yake ya kibiashara (Digitization Project) ikilinganishwa na hali ilivyokua mwaka 2021/2022. Maeneo ya vipaumbele muhimu katika mpango huo ni pamoja na;

i. Mfumo wa kisasa zaidi wa ERP,

ii. Jukwaa la kidijitali (ECM) kwaajili ya kuondokana na matumizi yote ya karatasi,

iii. Uunganishaji wa mifumo ya MSD na mifumo yote ya kisekta ikiwemo taasisi zinazofanya kazi na MSD kwa ukaribu,

iv. Mfumo wa ununuzi wa bidhaa za afya kwa nchi za SADC kwa njia ya kielektroniki (Electronic SADC Pool Procurement - eSPPS), na

v. Mfumo wa kusimamia mazingira ya ghala (Warehouse Environemt Monitoring System).

MSD tayari imeshaboresha matumizi ya mifumo ya kidijiti katika maeneo muhimu kama vile usimamizi wa mikataba na ufuatiliaji wa ununuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Bohari ya Dawa pia imeendelea kuimarisha matumizi ya mifumo ya TEHAMA kwa kusimika mfumo wa usimamizi na ufuatiliaji wa magari (Real time Fleet Management System), Mfumo wa “Proof of delivery” unaotumika kusainisha vituo baada ya kufikishwa mzigo vituoni na kupokelewa, na Customer Portal ambao hutumika na vituo vya kutolea huduma za afya kutambua bidhaa za afya zilizopo MSD na bei yake. Pamoja na hayo MSD tayari imeanza kazi ya ujenzi wa mfumo wa kisasa zaidi wa ERP wenye tija zaidi, ikiwa ni juhudi za kuhakikisha wateja wa MSD wanapata huduma bora kwa ufanisi zaidi na kwa kuzingatia usalama wa taarifa.

KUBORESHA MNYORORO WA UGAVI

Bohari ya Dawa ilikusudia kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za afya unaimarika, bidhaa za afya zinafika kwa wananchi kwa wakati na mabadiliko yanayotokea kwenye vituo vya kutolea huduma za afya yanafahamika MSD na hatua muhimu kuchukuliwa ili kuepusha ukosefu wa bidhaa za afya. Aidha, Bohari ya Dawa ilitambua umuhimu wa kujipanga na kuweza kukabiliana na majanga mbalimbali pindi yanapotokea na kuimarisha mifumo ili kuhakikisha bidhaa zinazopokelewa zinaendana na zile zilizoagizwa.

Hatua zilizofikiwa

i. Kuandaa mpango maalum wa ununuzi kutoka kwa wazalishaji wa ndani na wale wa nje;

ii. Kufanikisha bidhaa za huduma moja kutoka kwa mzabuni fanani ili kupunguza gharama za usimamizi na matengenezo, mfano; bidhaa zinazohusu uangalizi maalum kwa watoto kununuliwa kwa pamoja;

iii. Kugawanya majukumu kutoka kurugenzi moja na kuunda kurugenzi nyingine 2 (Kanda na huduma kwa wateja na Kurugenzi ya maghala na usimamizi wa mali) ili kuimarisha utendaji wa taasisi na kuweza kuhudumia wateja ipasavyo;

iv. Kufanya ugatuzi wa majukumu na kuwezesha Ofisi za Kanda kutekeleza majukumu mengi zaidi kwa kuhamisha baadhi ya shughuli zilizokuwa zikifanya Makao Makuu;

v. Kuanza kutekeleza mpango wa ununuzi kwa kuzingatia mahali ambapo bidhaa zinapatikana kwa urahisi;

vi. Kuendelea kusimamia na kuhakikisha bidhaa zote zinazozalishwa ndani ya MSD na zinazopokelewa kutoka kwa wazalishaji wengine zinakidhi ubora stahiki.

UTEKELEZAJI WA SERA YA VIWANDA

MSD imekuwa katika jitihada za kuanzisha viwanda vyake yenyewe kupitia mfumo wa Public Private Partnership (PPP) kwa mujibu wa Sheria ya PPP kwa kipindi kirefu lakini hatukufanikiwa kutokana na kukinzana kwa taratibu, masharti na namna ya utekelezaji wa mradi kwa mujibu wa sheria za PPP ikiwemo muda mrefu wa mradi na MSD kukosa umiliki katika uwekezaji. Hata hivyo, Mwaka 2021, Serikali ilifanya marekebisho ya Sheria ya Bohari ya Dawa na kuongeza rasmi jukumu la Uzalishaji Dawa na Vifaa tiba kwa MSD. Katika kutekeleza jukumu hili MSD ilifanya mageuzi makubwa ya kiusimamizi kwa kuanzisha Kampuni Tanzu “MSD Medipharm Manufacturing Co.LTD” ambayo inasimamia viwanda na jukumu la uzalishaji kwa asilimia 100 na ina mamlaka kisheria kuingia makubaliano ya ushirikiano na Kampuni mbalimbali za uwekezaji na kuwekeza pamoja.

UANZISHAJI WA KIWANDA CHA BARAKOA

Kufuatia mlipuko wa Uviko-19, Serikali iliamua kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuhakikisha vifaa kinga vya kuweza kuzuia maambukizi ya vimelea vinapatikana nchini. Mnamo mwaka 2021, Serikali kupitia Bohari ya Dawa ilisimika mitambo ya kuzalisha Barakoa za Kawaida ili kupambana na maambukizi ya Uviko-19. Kiwanda hiki kilichosimikwa kina uwezo wa kutimiza mahitaji ya nchi nzima. Aidha, katika kuhakikisha kwamba vifaa kinga hivi vinapatikana na kuweza kutumika hata maeneo hatarishi, mnamo mwaka 2023, Serikali kupitia MSD iliongeza mtambo mwingine wa uzalishaji wa Barakoa Maalum, N95, na kuweza kusimika Bohari ya Dawa. Barakoa aina hizi zinazalishwa kwa kiwango kinachokubaliwa na kupewa ithbati ya uzalishaji stahiki kutoka TMDA. Barakoa hizi zinaweza kukinga maambukizi dhidi ya vimelea hatarishi vya homa ya mapafu na maambukizi ya mfumo wa hewa. Kiwanda hiki pia kina uwezo wa kuzalisha wastani wa barakoa milioni 6 kwa mwaka na kukidhi mahitaji ya vituo vya kutolea huduma nchi nzima.

KUANZA UZALISHAJI WA MIPIRA YA MIKONO KATIKA KIWANDA CHA IDOFI

Mwezi Februari 2024, Serikali iliiwezesha MSD kukamilika kwa ujenzi wa Kiwanda pekee cha kuzalisha mipira ya mikono “Gloves” kilichopo Halmashauri ya Mji Makambako, Mkoani Njombe na kuanza uzalishaji. Kiwanda hiki kimegharimu fedha 15  kutoka Serikali ya kiasi cha shilingi bilioni 16. Kiwanda hiki kina uwezo wa kuzalisha wastani wa Gloves milioni 24.4 na kusaidia kukidhi zaidi ya asilimia 60 ya mahitaji ya bidhaa hii nchini na kupunguza uagizaji wa bidhaa hii kutoka nje ya nchi. Aidha viwanda hivi kwa sasa vipo chini ya Kampuni Tanzu ya MSD, MSD Medipharm Manufacturing Company Limited ambayo inasimamia Kiwanda cha Mipira ya Mikono Idofi - Njombe, eneo la viwanda la Zegereni - Pwani na Kiwanda cha Barakoa - Dar es Salaam pamoja na viwanda vya bidhaa za Afya zitokanazo na malighafi ya pamba na hivyo kupunguza uagiazaji wa bidhaa zitokanazo na pamba ambazo hugharimu nchini zaidi ya shilingi bilioni 25.

UPATIKANAJI WA MBIA WA UWEKEZAJI KATIKA UZALISHAJI WA BIDHAA ZA AFYA

Mnamo mwezi Oktoba 2024, Kampuni Tanzu ya Bohari ya Dawa inayoitwa MSD Medipharm Manufacturing Company Limited ilifanikiwa kusaini makubaliano ya uzalishaji wa bidhaa za afya kwa njia ya Joint Venture na Kampuni ya Rotabiogen East Africa inayomilikiwa na Kampuni ya Rotabiogen Egypt ya nchini Misri kwa dhumuni la kufanya uwekezaji na kuanza uzalishaji wa dawa za binadamu katika eneo la MSD lilipo Zegereni (Industrial Park for health commodities) na hivyo kwa pamoja kuanzisha Kampuni inayoitwa ROTAMEDI CO.LTD kwa utekelezaji wa mradi huu. Gharama za mradi huu zinatarajia kufika shilingi bilioni 183.3, sawa na Dola za Kimarekani milioni 72. Utekelezaji wa mradi huu umeanza mwezi Januari 2025 ambapo wataalamu kutoka Misri wamefika Tanzania na kukagua eneo la mradi na kuchukua taarifa kwa ajili ya kuanza usanifu wa mradi. Viwanda hivi vitakapokamilika vitapunguza uagizaji wa bidhaa za afya kutoka nje ya nchi zenye thamani ya shilingi bilioni 35 kwa mwaka, kutoa 16 mafunzo na ajira kwa Watanzania juu ya uzalishaji wa bidhaa za afya. Kampuni Tanzu ya MSD inaendelea kukamilisha uchambuzi wa athari za kimazingira (Enviromental and Social impact assessment) la eneo la mradi kama inavyoelekezwa na Baraza la Usimamizi wa mazingira (NEMC).

KUONGEZA UNUNUZI WA BIDHAA ZA AFYA KUTOKA KWA WAZALISHAJI WA NDANI

Serikali kupitia Bohari ya Dawa imeendelea kuongeza ununuzi wa bidhaa za afya kutoka kwa wazalishaji wa ndani ambapo kwa kipindi cha Julai-Disemba 2024/2025, bidhaa za afya zenye thamani ya shilingi bilioni 56.7 zimenunuliwa kutoka shilingi bilioni 22.1 zilizonunuliwa mwaka 2023/24 ikiwa ni ongezeko la asilimia 157. Dhamira hii itasaidia kuongeza uzalishaji na kuvutia wawekezaji ambapo matumizi ya fedha za kigeni yatapungua na ajira zitatengenezwa nchini.

UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUONGEZA MIUNDOMBINU

Serikali imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa kwa kuboresha huduma zinazotolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ikiwemo kuongeza huduma husika, kufanya upanuzi wa vituo na kujenga vituo vipya. Ongezeko la uwekezaji huu linaenda sambamba na ongezeko la idadi ya watu. Aidha, Serikali pia imekuwa ikihimiza matumizi ya nishati mbadala. Kutokana na maelekezo hayo, Bohari ya Dawa inatekeleza mradi wa wa kuboresha miundombinu unaohusu ujenzi wa maghala, ununuzi wa magari yanayotumia nishati ya gesi na umeme ili kuongeza ufanisi na usimikaji wa mifumo ya umeme wa jua katika ofisi na maghala yake. Miradi hii inatarajia kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 237.

UJENZI WA MAGHALA YA KUHIFADHI BIDHAA ZA AFYA

Kwa kutambua ongezeko la mahitaji na muelekeo wa kuwekeza kwenye nishati mbadala, Serikali kupitia Bohari ya Dawa imeanza ujenzi wa maghala mapya toka mwezi Agosti 2023 katika Kanda ya Mtwara na Dodoma ili kukidhi upungufu uliojitokeza. Ujenzi huu unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Machi 2025 na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 42. Fedha zinazotumika katika ujenzi wa maghala zimetolewa na Serikali. 17 Ghala linalojengwa Mtwara lina ukubwa wa mita za mraba 4,800 na lile lililopo Dodoma lina ukubwa wa mita za mraba 7200, hivyo kufanya ongezeko la uhifadhi kutoka mita za mraba 56,858.57 na kufikia mita za mraba 68,858.57. Miradi hii imekamilika kwa wastani wa asilimia 96. Kukamilika kwa miradi hii kutasaidia kuendana na ukuaji wa idadi ya watu na ongezeko la uwekezaji unaofanywa na Serikali kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, kupunguza gharama za uhifadhi na kuimarisha utunzaji wa bidhaa za afya kwa kuhakikisha bidhaa za afya zinahifadhiwa kwenye viwango vinavyokidhi mahitaji ya utunzaji salama wa bidhaa za afya na vituo vya kutolea huduma za afya zinapata bidhaa husika kwa wakati.

Ghala kuu la Dodoma litahudumia Kanda za Dodoma, Mwanza, Kagera, Iringa, Mbeya na Tabora kwa lengo la kuhakikisha bidhaa za afya zinapatikana za kutosha kwenye Kanda hizo na kwa wakati na kupunguza muda uliokuwa unapotea kufuata bidhaa za afya kutoka Dar es salaam. Pia, kukamilika kwa ghala hili kutapunguza gharama za uendeshaji wa taasisi kwakua kanda nufaika hazitafuata mizigo ghala kuu la Dar es Salaam, bali zitachukua mizigo yao kutoka ghala kuu la Dodoma hivyo kuhakikisha bidhaa za afya zinapatikana muda mwingi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Aidha, katika kuendeleza uwekezaji huu, Serikali ya awamu ya sita imeweza kutoka kiasi cha shilingi bilioni 16.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa ghala la kuhifadhi bidhaa za afya katika kanda ya Mwanza na shilingi bilioni 3.8 kwa kuwezesha kuanzisha ujenzi wa ghala la Chato mkoani Geita.

USIMIKAJI WA NISHATI MBADALA ITOKANAYO NA MFUMO WA NISHATI YA JUA

Serikali kupitia Bohari ya Dawa inatarajia kutekeleza mradi wa kuhifadhi mazingira kwa kutumia umeme wa jua “Green Project. Mradi huu kwa ujumla unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 36.6 na kiasi cha shilingi bilioni 13.8 kinatarajia kutolewa kwa ajili ya usimikaji wa nishati itokanayo na jua kwenye mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, 19 Tanga, Mtwara na Mwanza. Uwepo wa nishati hii itasaidia kuendana na mpango mzima wa Serikali wa kuhimiza matumizi ya nishati mbadala na utunzaji wa mazingira, utasaidia kuimarisha uhifadhi wa bidhaa za afya na kuokoa fedha nyingi zinazotumika katika shughuli za kila siku za Bohari ya Dawa.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.