MSD MBEYA, YAJADILIANA NA WADAU WAKE KUIMARISHA HUDUMA
Wateja wa MSD kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa, na halmashauri ya Makete Wahimizwa kutumia vyanzo vingine vya mapato kununua bidhaa za afya kutoka Bohari ya Dawa (MSD).
Aidha wametakiwa kulipa au kupunguza madeni yao wanayodaiwa na MSD ili kuipa nguvu ya kiuchumi katika mzunguko wa ugavi wa bidhaa za afya, badala ya kurundika madeni yao.