Aller au contenu principal

MSD YAKABIDHI JENERETA LA KVA 75 KWA HOSPITALI YA WILAYA YA KITETO

Hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara imeondokana na changamoto ya kukatiza baadhi ya huduma za matibabu kama upasuaji na pindi umeme unapokatika baada ya Bohari kuu ya dawa MSD kukabidhi jenereta lenye thamani ya shilingi milioni 65 itakayotumika kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano mjini Kibaya wilayani Kiteto, meneja wa MSD kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa amesema jenereta hilo lenye uwezo wa KVA 75 ni sehemu ya mahitaji ya vifaa vya afya vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 699 vilivyoagizwa na hospitali hiyo kwa bohari kuu ya dawa MSD katika mwaka wa fedha 2023/2024. 

Amesema tayari MSD imeshakabidhi vifaa vingine vilivyoagizwa katika hospitali hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni 683 sawa na asilimia 98 ya vifaa vilivyoagizwa na halmashauri hiyo kupitia MSD na ameahidi wakati wowote kuanzia sasa kukamilisha sehemu iliyobaki ambayo ni mfumo wa kuhifadhi miili (mortuary cabinet).  Mganga mkuu wa wilaya ya Kiteto Dkt Vicent Gyunda ameshukuru bohari kuu ya dawa kanda ya Dodoma kukabidhi jenereta hilo kwa wakati ambayo sasa   itawezesha uhakika wa huduma za upasuaji wa wagonjwa, kuwapa joto watoto njiti pamoja na huduma ya kuhifadhi maiti. 

Akizungumza katika hafla hiyo mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga ameagiza uongozi wa hospitali ya Halmashauri hiyo kutenga bajeti ya mafuta ya jenereta hilo ili litumike wakati wowote pindi umeme unapokatika. Wilaya ya Kiteto ni miongoni mwa maeneo ambayo huduma ya umeme hukatika kila mara kutokana na uchakavu wa miundombinu hali ambayo imekiwa ikitatiza utoaji wa huduma za kitabibu zinazohitaji uwepo wa umeme katika hospitali ya Halmashauri ya wilaya hiyo mjini Kibaya.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.