Aller au contenu principal
  • MSD YASHINDA TUZO TATU ZA MWAJIRI BORA 2024

    Bohari ya Dawa (MSD) imejinyakulia tuzo tatu za Mwajiri bora mwaka 2024 kupitia tuzo zinazotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

    Katika tuzo hizo zilizotolewa na Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dotto Biteko, MSD imeibuka na ushindi wa tuzo tatu ambazo ni pamoja na Taasisi bora kiutendaji (Club of Ten best performers), mshindi wa kwanza kwa taasisi inayotoa fursa za ajira (First runner up job creation na mshindi wa pili Mwajiri bora sekta ya umma (Second runner up Public Sector).

  • Mkoa wa Dodoma Wajipanga Kuboresha Upatikanaji wa Bidhaa za Afya

    Meneja MSD Kanda ya Dodoma Bi. Mwanashehe Jumaa ameuomba uongozi wa Timu ya Usiamizi wa afya Mkoa wa Dodoma (RHMT) kuratibu na kusimamia uwasilishwaji wa maombi ya mahitaji ya  vituo vya kutolea huduma za afya kwa wakati na ulipaji wa madeni, ili MSD iendelee kutoa huduma kwa ufanisi na kwa wakati.

  • Bohari ya Dawa (MSD) Kukuza Ushirikiano na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

    Bohari ya Dawa (MSD) imekutana ujumbe kutoka  Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) lengo likiwa kuanzisha ushrikiano wa kiutendaji kwenye nyanja za Utafiti, Ubunifu, Teknolojia, TEHAMA, Biashara na Fedha. Kikao hiko cha ushirikiano kimefanyika Makao Makuu ya MSD Keko Dar es Salaam,  huku kikikutanisha maafisa mbalimbali kutoka kwenye taasisi hizo. 

  • Ujumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Watembelea Hospitali za Mkoa wa Simiyu

    Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Bw. Ally Seleman, akiambatana na Kaimu Meneja Mipango,Tathimini na Ufuatiliaji leo tarehe 20/11/24 wametembelea Kanda ya MSD Mwanza na kujionea jinsi Kanda hiyo inavyotekeleza majukumu yake,  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MSD.

    Kupitia ziara hiyo Bw. Selemani amepokea taarifa ya utendaji wa Kanda hiyo, sambamba na mipango mbalimbali ambayo Kanda hiyo imejiwekea Ili kuhakikisha inaboresha huduma zake.

  • Ujumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Watembelea Kanda ya Mbeya

    Mwakilishi wa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Bohari ya Dawa (MSD), Dr. Alex Magesa, ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Ununuzi Hamis Mpinda wamefanya ziara katika Kanda ya MSD, Mbeya, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MSD.

    Katika ziara hiyo  viongozi  hao walitembelea wateja wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na kuzungumza nao kuweza kujua namna wanavyozipokea huduma za MSD na kujadili kwa pamoja namna ya kuboresha huduma hizo.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.