Aller au contenu principal
  • MSD na CRDB Wabadilishana Uzoefu

    Katika hatua ya kuongeza ujuzi katika utoaji wa huduma kwa wateja Watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) wa Kurugenzi ya Ugavi wanaofanya kazi kwenye Idara ya Huduma kwa Wateja wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Benki ya CRDB zilizopo jijini Dar es Salaam. 

    Lengo la ziara hiyo ni kubadilishana uzoefu na kujifunza namna Benki hiyo inavyotoa huduma kwa wateja wake na namna inavyoweza kusimamia na kutatua malalamiko ya wateja. 

  • MSD Yashiriki Shughuli za Kijamii na Kutembelea Wateja Wake, Ikiadhimisha Miaka 30 ya Utendaji Toka Ianzishwe

    Katika maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka huu 2024, ambayo yalienda sambamba na sambamba na shughuli za kuadhimisha miaka 30 ya MSD, jumla ya wateja 18 walitembelewa kupitia kanda zote za MSD na kujadiliana masuala mbalimbali ya kuboresha huduma zinazotolewa na MSD pamoja na mahusiano na ushirikiano na wateja.

  • Mganga Mkuu Mkoa wa Pwani, Apongeza Ushirikiano Baina ya MSD na Wateja Wake.

    Bohari ya Dawa(MSD) Kanda ya Dar es Salaam imeandaa kikao kazi na wadau wake wa mkoa wa Pwani kilichofanyika Mkoani Pwani - Wilayani Kabaha katika Chuo cha Mwalimu Nyerere  kuzungumza kwa pamoja namna ya koboresha upatikanaji wa bidhaa za afya.

    Akizungumza kwenye kikao hicho Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dkt. Urio Kusirye amesema vikao kazi hivyo ni muhimu kwani vinachangia kuhakikisha huduma za afya ndani ya Mkoa wa Pwani zinakuwa endelevu na bora.

  • Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi MSD, Watembelea Mbuga ya Taifa ya Tarangire

    Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Bohari ya Dawa (MSD) wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire lengo likiwa ni kujionea vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ambayo inapatikana ndani ya mkoa wa Manyara.

    Ziara hiyo imekuja ili kuongeza chachu na kuhamasisha wageni na watumishi mbalimbali kuweza kutembelea vivutio vyetu vya utalii vilivyoko nchini, ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Kutangaza utalii nchini.

  • Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, Aipongeza MSD kwa Manunuzi Vifaa Tiba vya Mama na Mtoto

    Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa kuendelea kuhakikisha inanunua vifaa muhimu vinavyohitajika kusaidia kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa wakiwa Njiti.

    Waziri Mhagama amesema hayo leo wakati akikabidhi vifaa tiba maalumu vya kuwasaidia watoto wenye matatizo kupumua, ambavyo amevikabidhi kwa  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Dkt. Mohammed Mang'una kwa niaba ya Waganga Wakuu wote nchini. 

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.