Serikali Yamwaga Vifaa Tiba vya Milioni 222.472 Mkoani Singida
SERIKALI ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi vifaa tiba Mkoa wa Singida vyenye jumla ya takribani Sh.Milioni 222.472, kwaajili ya kuboresha huduma za afya Mkoani humo.
Vifaa hivyo ni pamoja na majenereta, sambamba na vifaa vitakavyotumika kuhudumia watoto wanaozaliwa kabla ya muda na huduma nyinginezo ambavyo vimekabidhiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Ikungi, Kituo cha Afya Sepuka na Hospitali ya Wilaya ya Singida, Ilongero.