RMO Manyara - Avitaka Vituo vya Kutolea Huduma za Afya Kulipa Madeni ya MSD,
Watendaji kwenye vituo vya kutolea huduma za afya waliopo kwenye Mkoa wa Manyara wamekumbushwa kuendelea na utaratibu wa kulipa madeni ya Bohari ya dawa (MSD) kwani kufanya hivyo ni kuiwezesha MSD kuwa na mtaji mzuri wa kuendelea kununua bidhaa za afya ambazo zinasambazwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Andrew Method alipokuwa anafungua kikao cha wadau na wateja wa MSD kanda ya Kilimanjaro wa mkoani wa Manyara.