Serikali Kupitia MSD Kanda ya Dar es Salaam Yasambaza Vifaa Tiba vya Milioni 930 - Wilaya ya Ulanga.
SERIKALI kupitia Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Dar es Salaam imesambaza vifaa tiba vya zaidi ya sh. milioni 930 kwa ajili ya vituo vya afya 24 vya halmshauri ya Wilaya ya Ulanga.
Akizungumza jana Wilayani humo mkoani Morogoro Mbunge wa jimbo la Ulanga Salim Hasham, alisema, wamepokea vifaa tiba hivyo na dawa za zaidi ya sh. milioni 900 kwa ajili ya vituo vya afya 23 vya halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.