MSD Yakabidhi Vifaa vya Upasuaji Vyenye Thamani ya Milioni 210, Itigi
Bohari ya Dawa (MSD) kupitia Kanda ya Dodoma leo imekabidhi vifaa vya upasuaji kwa hospitali ya Wilaya ya Itigi, iliyoko mkoani Singida, vyenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 210.
Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Dkt.Vicent Mashinji amesema nia ya serikali kununua vifaa hivyo ni kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa viwango vinavyokubalika, na kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika hasa kwa mama na watoto wakati wa kujifungua.