Skip to main content

Utunzaji

Bohari ya Dawa inatunza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye maghala yake ambayo yapo kimkakati katika mikoa tofauti kote nchini. Katika kipindi cha miaka sita iliyopita, Bohari ya Dawa imeboresha maghala yake kwa kuyaunganisha na mifumo ya teknolojia ya kisasa ya uhifadhi. Hivi sasa Bohari ya Dawa ina mita za mraba 42,038.38 ambazo zinajumuisha magahala takribani 10 yaliyopo kwenye Kanda zote za MSD katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Iringa, Kilimanjaro, Mbeya, Tabora, Dodoma, Mtwara, Tanga na Kagera.

Bohari ya Dawa imefanikiwa kuongeza uwezo wa kutunza dawa na vitendanishi vinavyohitaji kutunzwa kwenye ubaridi, kwa kuongeza miundombinu ya uhifadhi wa dawa za mnyororo baridi, mpaka kufikia jumla ya mita za mraba 1,000. Maghala ya kisasa ya MSD (Warehouse in -a- Box (WiBs)) yaliyopo Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Tabora, Dodoma na Tanga yameongeza uwezo wa uhifadhi, kiwango cha huduma na usahihi wa taarifa.

Katika kukabiliana na changamoto za utunzaji na ufuatiliaji wa kumbukumbu wakati wa kupokea, kuhifadhi na kutoa bidhaa, Bohari ya Dawa pia imeweka mfumo wa kutumia Msimbo Mpau (Barcode) ili kupata taarifa za bidhaa  kupitia mfumo wa kielektroniki. Matumizi ya Msimbo Mpau (Barcode) yamepunguza mlolongo wa majukumu kwa watumishi wa ghalani katika kupata taarifa na takwimu sahihi kwa ajili ya kuhifadhi na kutoa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara ghalani, usahihi wa takwimu za mali ghalani, pia kurahisisha ufuatiliaji wa taarifa za muhimu za uhifadhi.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.