Skip to main content

MSD Yashiriki Shughuli za Kijamii na Kutembelea Wateja Wake, Ikiadhimisha Miaka 30 ya Utendaji Toka Ianzishwe

Katika maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka huu 2024, ambayo yalienda sambamba na sambamba na shughuli za kuadhimisha miaka 30 ya MSD, jumla ya wateja 18 walitembelewa kupitia kanda zote za MSD na kujadiliana masuala mbalimbali ya kuboresha huduma zinazotolewa na MSD pamoja na mahusiano na ushirikiano na wateja.

Akizungumza baada ya shughuli hizo Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji Victor Sungusia ameeleza kuwa, kwa kuwa MSD inathamini mchango mkubwa wa mawazo yanayotolewa na wateja wake katika kufanya maboresho ya utoaji huduma, waliamua kuwafuata vituoni, badala ya kusubiri mikutano ya wadau ili pia kujionea hali halisi ya huduma wanazotoa, hasa kupata mrejesho wa vifaa walivyosambaza.

Katika maeneo yote ya wateja yaliyotembelewa na MSD, wadau na wateja wa MSD wameeleza kuridhishwa kwao na juhudi za uongozi wa MSD kufanya maboresho ya huduma na kiutendaji kwa ujumla, wakirejea hali halisi ya kuridhika kwa upatikanaji wa bidhaa za afya vituoni, ambao hadi sasa kwa wastani umefikia asilimia 92.

Aidha wateja hao wameeleza kuridhishwa na mifumo ya mawasiliano baina yao na MSD, ubora wa bidhaa za afya zinazonunuliwa na kusambazwa na MSD, bidhaa za afya kufika kwa wakati, kuimarisha mifumo ya mnyororo wa ugavi tangu kuomba bidhaa za afya hadi kupokea na kuleta vifaa na mashine za kisasa ambazo awali ilikuwa tabu kuzipata.

Mbali na kutembelea wateja, baadhi ya wateja wa MSD walitembelea Kanda zetu na kujionea namna MSD inavyotekeleza majukumu yake ya mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya, ambapo pia walitembelea maghala ya kuhifadhia bidhaa za afya na kuona shughuli nzima za kupokea na kuhifadhi na kutoa bidhaa za afya zinavyofanywa ghalani.

Mara baada ya ziara zote mbili, MSD pamoja na wadau na wateja wao kwa pamoja walikata keki na kula pamoja, kama ishara ya kuimarisha ushirikiano baina ya pande hizo mbili. Baadhi ya Kanda pia zilikabidhi bidhaa za afya zilizokuwapo kwenye kalenda ya mgawo, kukabidhi zawadi mbalimbali, misaada na kupata chakula cha pamoja na wadau.

Katika hatua nyigine Kanda zote za MSD, zilishiriki matendo ya huruma kwa kutoa misaada mbalimbali ya kijamii kwa wahitaji (CSR) katika hospitali 

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.