Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Atoa Rai - Matumizi ya Vyandarua
Kongwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius M. Emmanuel amewataka wakazi na wazazi wote wilayani humo kutumia vyema na kwa lengo lililokusudiwa vyandarua vya msaada wanavyopatiwa serikali, ili adhima ya serikali ya kupambana na ugonjwa wa Malaria iweze kutimia.
Mhe. Remidius ametoa rai hiyo hii leo wakati akizindua rasmi zoezi la usambazaji wa vyandarua mashuleni wilayani humo, linalofanya na Bohari ya Dawa (MSD).