Skip to main content

Sisi ni Nani

Bohari ya Dawa (MSD) ni idara chini ya Wizara ya Afya ambayo ilianzishwa mwaka 1993 kwa Sheria ya Bohari ya Dawa, Sura. 70 kama ilivyorekebishwa mwaka 2021. MSD ina jukumu la kuandaa, kutunza na kusimamia mfumo bora na wa gharama nafuu za usazalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa dawa na vifaa tiba vinavyohitajika kwa matumizi ya vituo vyote vya afya vya umma.

Bodi ya Wadhamini ndicho chombo cha juu cha maamuzi kinachosimamia na kuweka mwelekeo wa MSD kwa niaba ya Wizara ya Afya. Bodi inaundwa na wajumbe tisa (9) wanaoteuliwa kila baada ya miaka mitatu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye anayemteua Mwenyekiti, na Waziri mwenye dhamana ya afya huteua wajumbe wengine (8). Mkurugenzi Mkuu anahudumu kama Katibu wa Bodi lakini hana haki ya kupiga kura.

Ili kuhakikisha utekelezaji mzuri wa majukumu yake, Bodi ya Wadhamini inaendesha kazi zake kupitia Kamati tatu za Bodi ambazo ni; Kamati ya Ukaguzi na Vihatarishi, Kamati ya Huduma za Kiufundi, na Kamati ya Fedha na Utawala. Bodi inakasimu usimamizi wa kila siku wa MSD kwa Mkurugenzi Mkuu, ambaye huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kazi za usimamizi na uendeshaji wa MSD hufanywa kupitia Menejimenti (EMT) ambayo inaundwa na Mkurugenzi Mkuu (Mwenyekiti) na Wakurugenzi wengine.

Mkuu wa Kitengo cha Sheria anahudumu kama Katibu wa Menejimenti ya MSD. MSD huendesha shughuli zake kupitia Kanda kumi (10) ambazo ni Dar es Salaam, Mwanza, Iringa, Kilimanjaro, Mbeya, Tabora, Dodoma, Tanga na Mtwara na Kagera.

Aidha, ili kuimarisha upatikanaji wa dawa karibu na wananchi, MSD ilianzisha maduka ya dawa (MCOs) yaliyopo katika mikoa mbalimbali ya Dar es Salaam katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mbeya jirani na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, Geita katika hospitali ya Wilaya ya Chato, na Hospitali ya Katavi katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.