MSD na CRDB Wabadilishana Uzoefu
Katika hatua ya kuongeza ujuzi katika utoaji wa huduma kwa wateja Watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) wa Kurugenzi ya Ugavi wanaofanya kazi kwenye Idara ya Huduma kwa Wateja wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Benki ya CRDB zilizopo jijini Dar es Salaam.
Lengo la ziara hiyo ni kubadilishana uzoefu na kujifunza namna Benki hiyo inavyotoa huduma kwa wateja wake na namna inavyoweza kusimamia na kutatua malalamiko ya wateja.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja wa CRDB Yolanda Urio amesema, leo tumewakaribisha MSD hapa kwetu tunachotamani wao kukifahamu ni kwamba kutoa huduma sio tu jukumu letu bali ni shauku yetu pia. Benki ya CRDB tunachukulia kila mazungumzo ni fursa ya kuongeza matarajio na uhusiano wa kiuchumi.
Kwa upande wake Meneja Huduma kwa Wateja wa MSD Dkt. Pamella Sawa amesema kwasasa MSD ipo kwenye mkakati wa kuboresha Idara yake ya Huduma kwa Wateja ili kuendana na mpango wa MSD kujiendesha kibiashara.
MSD sasa inahudumia zaidi wateja 8,500 nchi nzima hivyo tunahitaji njia sahihi za kuwahudumia wateja hao wote ili kuhakikisha wanafurahia huduma za MSD. “ Pamoja na mambo mengine ziara hii itaboresha mahusiano baina ya CRDB na MSD ameongeza Dkt. Sawa.
- Log in to post comments