Ujumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Watembelea Kanda ya Mbeya
Mwakilishi wa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Bohari ya Dawa (MSD), Dr. Alex Magesa, ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Ununuzi Hamis Mpinda wamefanya ziara katika Kanda ya MSD, Mbeya, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MSD.
Katika ziara hiyo viongozi hao walitembelea wateja wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na kuzungumza nao kuweza kujua namna wanavyozipokea huduma za MSD na kujadili kwa pamoja namna ya kuboresha huduma hizo.