Skip to main content
  • Wizara ya Afya nchini Somalia waja kujifunza MSD

    Wizara ya Afya nchini Somalia imeichagua  Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kushirikiana kwenye masuala mbalimbali yanayohusu mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya kwa  kubadilishana uzoefu katika maeneo ya mifumo, ununuzi, usambazaji na udhibiti ubora.

  • Bidhaa za Mama na Mtoto

    Hadi kufikia mwaka 2025 MSD tayari imekamilisha ununuzi na usambazaji wa vifaa tiba vya kupambana na vifo vya uzazi pingamizi CEmONC kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. MSD imeweza kufanya ununuzi wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tzs. 100,182,390,897.40 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya 414. Katika vifaa tiba hivi asilimia themanini (80) imejikita katika vifaa vya upasuaji kama taa za upasuaji, mashine za usingizi, vitanda vya upasuaji ambavyo vimeenda okoa Maisha ya wamama na Watoto nchini Tanzania.

  • Uzalishaji wa Bidhaa za Afya

    Katika kuongeza ufanisi wa usimamizi wa shughuli za uzalishaji na kuhakikisha utekelezaji wa miradi kwa wakati, MSD imeanzisha Kampuni Tanzu inayoitwa “MSD Medipharm Manufacturing Company Limited” ambayo inajukumu la kusimamia shughuli za uzalishaji wa bidhaa za afya na itakuwa na uwezo wa kuingia ubia na wawekezaji wengine. Kwa sasa kampuni hii inasimamia viwanda vya Barakoa (Surgical na N95 Mask) Dar es salaam na kiwanda cha Mipira ya Mikono Idofi Makambako, Mkoani Njombe.

  • Huduma za MSD kwa vituo vya afya

    Toka MSD ianzishwe mwaka 1994 ilikuwa ikihudumia vituo vya kutolea huduma za afya takribani 200- 500 nchi nzima. Kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma za afya Serikali na watu binafsi wamekuwa wakijenga vituo vya kutolea huduma sehemu mbalimbali ya nchi ambapo  hadi sasa wateja wa MSD ni zaidi ya 8,500. 

    Ongezeko hili linaifanya MSD kuendelea kutanua huduma zake za uzalishaji, utunzaji manunuzi, usambazaji.

  • MSD Yakabidhi Vifaa vya Upasuaji Vyenye Thamani ya Milioni 210, Itigi

    Bohari ya Dawa (MSD) kupitia Kanda ya Dodoma  leo imekabidhi vifaa vya  upasuaji kwa hospitali ya Wilaya ya Itigi, iliyoko mkoani Singida, vyenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 210.

    Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Dkt.Vicent Mashinji amesema nia ya serikali kununua vifaa hivyo ni kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa viwango vinavyokubalika, na kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika hasa kwa mama na watoto wakati wa kujifungua.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.