Mhe. Ummy Mwalimu Azindua Bodi Mpya ya Wadhamini ya MSD.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo amezindua Bodi mpya ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) na kuwaelekeza wajumbe hao Bodi kuhakikisha wanawezesha kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya zenye ubora na bei nafuu.
Waziri Ummy amewaeleza wajumbe hao wa Bodi ya Wadhamini kuwa watapimwa kwa kuangalia hali halisi ya upatikanaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.