MSD Kilimanjaro Yajadili Mbinu Kuboresha Uhusiano na Huduma kwa Wateja
ARUSHA.
MSD Kanda ya Kilimanjaro imekutana na wateja wake wanaopata huduma kutoka Kanda hiyo ambao ni kutoka mikoa yaArusha, Kilimanjaro na Manyara, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanagusa pande hizo, kwa lengo la kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
Mkutano huo wa siku moja umefanyika Mkoani Arusha ukiwa na lengo la kujenga uhusiano mzuri baina ya MSD Kanda ya Kilimanjaro na wateja wake wote wanaohudumiwa na Kanda hiyo.
Akifungua Mkutano huo Kaimu mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bi. Vones Uisso, amesema mkutano huo utawawezeshaMSD kupokea maoni na ushauri utakaochangia kuboresha huduma ambazo wanazitoa kwa wateja wake.
Ameongeza kuwamkutano huu utawezesha MSD kujadiliana namna nzuri ya kufanya kazi kwa pamoja na wateja wake ili kila mmoja awezekutimiza wajibu wa kumhudumia mwananchi.
Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Kilimanjaro Bi. Rehema Shelukindo amesema mkutano huu wa wateja utadumishaumoja, ambao utaendelea kuwezesha kuwahudumia wananchi kwa wakati.
Ameongeza kuwa mkutano huo utawezeshakupokea maboresho ambayo wateja wanawasilisha na kuyafanyia kazi.
- Log in to post comments