Waelimisha Rika MSD Wanolewa
Dar es salaam
Waelimisha rika (Pear Educators) ambao ni Watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) wanapatiwa mafunzo ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya UKIMWI pamoja na magonjwa yasiyoambukiza.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanahusisha waelimika rika kutoka Kanda na Idara zote za MSD, ambao watakuwa waelimishaji watumishi wengine.
Sera ya MSD ya kukinga watumishi dhidi ya UKIMWI na magonjwa yasiyoaambukiza inaeleza kuwa kila Kanda na Idara ya MSD inatakiwa kuwa na mueleimisha rika ili aweze kuwasaidia watumishi wengine namna ya kujikinga dhidi ya UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza.
Mkufunzi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Kweka amesema Elimu ya UKIMWI mahali pa kazi inawawezesha watumishi kuzingatia mihimili muhimu kuwa na uhakika wa elimu na habari za magonjwa tajwa, mafunzo,ufahamu wa kupima kwa hiari, matunzo na kusaidia waathirika.
Aidha watumishi watakuwa chachu katika kampeni ya kujikinga na kudhibiti magonjwa hayo.
- Log in to post comments