Madereva wa MSD Wajengewa Uwezo
MOROGORO.
Watumishi wa MSD wa kada ya Udereva, wameendelea kujengewa uwezo kupitia mafunzo mbalimbali, yanayoandaliwa na taasisi mathalani udereva wa kujihami, alama za barabarani, ukaguzi wa magari, sheria za usalama barabarani, upakiaji wa mizigo na namna bora ya kuendesha magari makubwa yanayovuta tella (truck and trailers) ili kuongeza tija katika kazi zao na taasisi kwa ujumla.
Mafunzo hayo ya siku 10 yamehusisha nadharia na vitendo na yametolewa na wataalamu kutoka Chuo cha Ufundi Veta, kilichoko Mkoani Morogoro.
Kwaupande wake Mkufunzi wa Chuo hicho Bw. William Emmanuel Munuo, ambaye amekuwa akiendesha mafunzo hayo ameipongeza MSD kwa kuratibu mafunzo hayo, kwani yamekua na tija kwa wanafunzi wake.
"Teknolojia zinabadilika katika magari, alama za usalama zinaongezeka, barabara zinabadilika, hivi sasa nchini zipo barabara za juu na chini, hivyo ni vyema kuwanoa maderava wetu ili waweze kwenda na wakati, niwapongeze MSD kwa kuliona hilo" Alisema Bw.Mnuo
Akizumgumza kwaniaba ya Maderava wa MSD Bw. Marwa Wangwe, amesema mafunzo hayo yamewaongezea ujuzi, kujiamini na uelewa wa masuala mbalimbali ya muhimu katika uedenshaji wa vyombo vya moto.
Aidha ameiomba Menejimenti ya MSD, kuratibu mafunzo hayo mara kwa mara, ili kuwajengea uwezo na kuongeza tija katika utekelezaji wa shughuli za taasisi.
- Log in to post comments