Watumishi wapya MSD Wapatiwa Mafunzo ya Mifumo
Watumishi wapya MSD wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutumia mifumo ya kiutendaji ya MSD ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.
Mafunzo hayo yanayofanyika MSD Keko jijini Dar es Salaam ni ya siku kumi na yanahusisha mifumo yote ambayo watumishi hao wataitumia katika kutoa huduma kwa wateja na wadau mbalimbali wa MSD.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkufunzi wa mafunzo hayo Emmanuel Mnzava ambaye ni Afisa TEHAMA Mkuu wa MSD amesema kila mtumishi anaeajiriwa au kuhamishiwa MSD anapaswa kupata mafunzo ya namna ya kutumia mifumo mbalimbali ya kiutendaji ambayo itamuwezesha katika utoaji wa huduma kwa ufasa.
Mnzava ameongeza kuwa mifumo ndio nyenzo kubwa inayowezesha MSD kuendesha shughuli zake za kila siku ikiwemo kuhudumia wateja na wadau wake, pia kuhifadhi kumbukumbu za taasisi.
- Log in to post comments