Skip to main content

BOHARI YA DAWA ( MSD) IMEINGIA MAKUBALIANO NA JESHI LA POLISI TANZANIA

Bohari ya Dawa ( MSD) imeingia makubaliano na Jeshi la Polisi Tanzania yanayolenga  kuimarisha ulinzi na usalama wa bidhaa za afya zinazosambazwa na MSD nchini. Makubaliano hayo pia yamelenga kusimamia kikamilifu mfumo wa usafirishaji wa bidhaa za afya na hivyo kuufanya kuwa salama na kuhakikisha bidhaa za afya zinafika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya zikiwa salama.  

Akizungumza kwenye tukio la kutia saini makubaliano hayo Kamishina wa Oparesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi, Awadhi Juma Haji, amesema Makubaliano haya ni hatua muhimu katika kuimarisha usimamizi wa usafirishaji wa bidhaa za afya, lakini pia  kufunga mianya ya uharibifu na wizi wa mali.  “Hii ni hatua kubwa na sisi kama jeshi la polisi tutahakikisha kazi hii inafanyika kikamilifu kwakuwa bidhaa zinazosambazwa na MSD ni mali ya serikali na mnufaika mkuu ni mwananchi hivyo zinapaswa kulindwa kikamilifu aliongeza ndugu Haji”.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Mavere Tukai amesema kutokana na kukua na kupanuka kwa majukumu ya MSD  kuna umuhimu wa kuimarisha mahusiano na jeshi la polisi kwenye majukumu mbalimbali yanayofanywa na MSD.  “Tunategemea ushirikiano huu wa Jeshi la Polisi na MSD utakwenda kudhibiti mianya yote ya upotevu wa bidhaa za afya na kuhakikisha usalama wa dawa zinazohitajika kwa afya ya Watanzania.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.