Wanamichezo wa MSD Watoa Msaada wa Kijamii Kituo cha Afya Ngamiani
Wanamichezo wa Bohari ya Dawa (MSD) wanaoshiriki kwenye mashindano ya SHIMUTA 2024 mkoani Tanga wametumia siku ya leo ya mapumziko kutembelea Kituo cha afya Ngamiani kilichopo mkoani Tanga na kutoa msaada wa bidhaa za afya kwa Wodi ya mama na mtoto.
Muuguzi Mkuu wa Kituo hiko Ndugu. Bahati Shiminogeni amewashukuru wanamichezo hao kwa msaada huo na kusema msaada uliotolewa ni muhimu kwani unakwenda kuwasaidia kwenye matumizi yao ya usafi pale wanapokuwa wanapata huduma wodini. “Nimefurahishwa na wanamichezo wa MSD kwani Mkoa wa Tanga kwa sasa kuna wanamichezo wengi lakini nimeshangaa kuona wachezaji wa MSD kutembelea na kujionea namna huduma zinavyotolewa hapa kituoni kwetu” aliongeza Shiminigeni.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Meneja wa MSD Kanda ya Tanga Ndg. Grant Mwapele amesema wanamichezo wa MSD wameamua kutoa msaada huu wa bidhaa za afya ndogondogo ikiwemo mafuta ya kujipaka, nepi (pampers) sabuni na wipers ambazo zitawasaidia akina mama na watoto katika usafi pindi wawapo wodini.
Hata hivyo, Ndg. Mwapele amewaeleza watumishi hao kuwa MSD ina bidhaa za afya za kutosha zikiwemo vitanda na magodoro hivyo wanaweza kuagiza pale wanapokuwa na changamoto ya upungufu au uchakavu wa bidhaa hizo ambazo ni muhimu kwa kituo hicho.
- Log in to post comments