Skip to main content

MSD Yashiriki Michuano ya SHIMUTA 2024

Wachezaji wa Bohari ya Dawa (MSD) watakaoshiriki kwenye mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma,Taasisi na Makampuni Binafsi (SHIMUTA)  mwaka 2024 jijiniTanga, leo Ijumaa tarehe 8 Novemba 2024 wameagwa na Menejimenti ya MSD na kuanza safari ya kuelekea kwenye mashindano hayo. 

Akizungumza wakati wa kuwaaga wachezaji hao Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Elisamehe Macha amewakumbusha watumishi hao kuwa michezo ni sehemu ya kazi hivyo wanapaswa kuhakikisha wanaenzi tunu za MSD ikiwemo uhodari na nidhamu kama wanapokuwa sehemu zao za kazi. 

“Tunategemea kuona mnajituma ikibidi kupata ushindi, MSD inathamini na kuwekeza kwenye michezo kwa kuwa michezo ni afya kwa watumishi wetu na inapelekea kuleta tija kwenye utendaji wa watumishi wa MSD. Mnapokuwa michezoni msisahau kuzingatia nidhamu kwa kuwa mnabeba taswira ya taasisi.

Macha, amewaeleza kuwa Menejimenti ya MSD inapenda michezo ifanyike kwa umahiri kwani MSD tumeanza kushiriki mashindano haya ya SHIMUTA, tujipange vizuri  ili kuhakikisha MSD inashiriki vizuri zaidi kwenye michezo hii pamoja na  mingine ijayo kwa kufanya maandalizi ya mapema na kuweka mfumo mzuri wa kutambua vipaji vya watumishi.

MSD imepeleka wachezaji hamsini na tisa (59)  kushiriki michezo mbalimbali katika mashindano ya mwaka huu ya SHIMUTA

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.