Skip to main content

Ujumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Watembelea Hospitali za Mkoa wa Simiyu

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Bw. Ally Seleman, akiambatana na Kaimu Meneja Mipango,Tathimini na Ufuatiliaji leo tarehe 20/11/24 wametembelea Kanda ya MSD Mwanza na kujionea jinsi Kanda hiyo inavyotekeleza majukumu yake,  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MSD.

Kupitia ziara hiyo Bw. Selemani amepokea taarifa ya utendaji wa Kanda hiyo, sambamba na mipango mbalimbali ambayo Kanda hiyo imejiwekea Ili kuhakikisha inaboresha huduma zake.

Bw. Selemani ameipongeza Kanda hiyo kwa jinsi inavyotekeleza majukumu yake, licha ya eneo kubwa inalohudumia, huku akiahidi kutafutia ufumbuzi baadhi ya changamoto zinazoikabili Kanda hiyo, ili kuongeza ufanisi zaidi.

Katika hatua nyingine ujumbe huo wa MSD, ukiongozwa na Bw. Selemani umetembelea hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Simiyu, sambamba na Hospitali ya Wilaya ya Bariadi  kutathimini hali ya upatikanaji wa huduma za MSD Mkoani hapo.

Akimzungumza wakati wa ziara hiyo Mganga Mfawidhi wa hospitali Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Dkt. Athanas Ngambakubi ameipongeza MSD kwa kuboresha huduma zake, ukilinganisha na kipindi cha nyuma kwani hivi sasa upatikanaji wa Dawa na Vifaa tiba umeimairika kwa zaidi ya asilimia 70 hospitalini hapo.

Aidha amebainisha kwamba Ubora wa bidhaa za MSD umekuwa wa uhakika, huku gharama ya bidhaa hizo ikiwa ni rafiki zaidi kuliko washitiri wengine.

Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Bariadi Dkt. Maghembe Kuligwa amebaisha upatikanaji wa bidhaa za afya hospitalini hapo kuwa zaidi ya asilimia 90, huku akipongeza MSD kwa kuboresha huduma zake, mathalani usambazaji wa Dawa sambamba na upatikanaji wa Vifaa tiba, ulikilinganisha miaka ya nyuma.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.