Skip to main content

Ujumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Watembelea Kanda ya Mbeya

Mwakilishi wa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Bohari ya Dawa (MSD), Dr. Alex Magesa, ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Ununuzi Hamis Mpinda wamefanya ziara katika Kanda ya MSD, Mbeya, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MSD.

Katika ziara hiyo  viongozi  hao walitembelea wateja wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na kuzungumza nao kuweza kujua namna wanavyozipokea huduma za MSD na kujadili kwa pamoja namna ya kuboresha huduma hizo.

Akizungumza baada ya ziara hiyo mjumbe huyo wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Dr. Magesa amesema kuwa wameweza kutembelea ghala la kanda ya Mkoa wa Mbeya na kujionea jinsi shughuli za ugavi wa bidhaa za afya zinavyofanyika.

Dr. Magesa ameeleza kuwa,  amefurahishwa na ari ya watumishi wa MSD Kanda ya Mbeya na utendaji wao ambapo umeonyesha kiwango cha juu cha juhudi na weledi.

Naye Mkurugenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji ameishukuru MSD kwa huduma bora wanazotoa na ushirikiano wa karibu ambao umesaidia hospitali hiyo kupata bidhaa za afya kwa wakati zikiwa na ubora unaostahili.

Naye Kaimu Meneja wa MSD Kanda ya Mbeya, Petro Mdegela, amesema ziara hiyo pia itahusisha kituo cha afya na zahanati ili kuweza kupata mrejesho wa huduma zinazotolewa na MSD katika ngazi zote za vituo vya kutolea huduma za afya.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.