MSD Yatunukiwa Tuzo na Shule ya Famasia (MUHAS)
Shule ya Famasia (MUHAS) imeitunuku Bohari ya Dawa (MSD) tuzo ya uhusiano mzuri wa kiutendaji pamoja ma ushirikiano.Tuzo hiyo imetolewa katika maadhimisho ya miaka 50 ya Shule hiyo na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Ndg. Mavere Tukai kwa niaba ya watumishi wa MSD.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Ndg. Mavere amesema MSD ni mdau wa shule ya famasia na imekua ikitoa ushirikiano kutoa mafunzo ya nadharia kwa wanafunzi katika ngazi mbalimbali.
Ameongeza kuwa MSD inaendelea kupokea wanafunzi wanaohitaji kupata taarifa na mafunzo kuhusu mnyororo wa ugavi kwenye sekta ya afya na upatikanaji wa bidhaa za afya hususan dawa.
Pamoja na kupatiwa tuzo hiyo MSD ikiwa mdau mkubwa katika utoaji wa huduma za ununuzi wa bidhaa za afya kwa wananchi inashiriki kwenye maonesho yaliyoandaliwa na shule hiyo huku ikionesha kwa wananchi namna inavyotekeleza majukumu yake ya Uzalishaji, Ununuzi.
Kwa upande wake Meneja Huduma kwa Wateja wa MSD Dkt. Pamella Sawa, amesema kupitia maonesho haya MSD imeendelea kutoa elimu juu ya bidhaa mbalimbali ambazo kwa sasa zinazalishwa kupitia viwanda vyake lakini pia bidhaa mbalimbali ambazo MSD inazinunua kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma vya afya nchini.
“Ninapenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wananchi wote kuja kwenye banda la MSD kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ambayo MSD imeandaa kwa ajili yao”. Alisema Dkt. Sawa.
- Log in to post comments