Aller au contenu principal
  • Waelimisha Rika MSD Wanolewa

    Dar es salaam

    Waelimisha rika (Pear Educators) ambao ni Watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) wanapatiwa mafunzo ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya UKIMWI pamoja na magonjwa yasiyoambukiza. 

    Mafunzo hayo ya siku tatu yanahusisha waelimika rika kutoka Kanda na Idara zote za MSD, ambao watakuwa waelimishaji watumishi wengine.

  • Watumishi wapya MSD Wapatiwa Mafunzo ya Mifumo

    Watumishi wapya MSD wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutumia mifumo ya kiutendaji ya MSD ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.

    Mafunzo hayo yanayofanyika MSD Keko jijini Dar es Salaam ni ya siku kumi na yanahusisha mifumo yote ambayo watumishi hao wataitumia katika kutoa huduma kwa wateja na wadau mbalimbali wa MSD. 

  • Madereva wa MSD Wajengewa Uwezo

    MOROGORO.

    Watumishi wa MSD wa kada ya Udereva, wameendelea kujengewa uwezo kupitia mafunzo mbalimbali, yanayoandaliwa na taasisi mathalani udereva wa kujihami, alama za barabarani, ukaguzi wa magari, sheria za usalama barabarani, upakiaji wa mizigo na namna bora ya kuendesha magari makubwa yanayovuta tella (truck and trailers) ili kuongeza tija katika kazi zao na taasisi kwa ujumla.

    Mafunzo hayo ya siku 10 yamehusisha nadharia na vitendo na yametolewa na wataalamu kutoka Chuo cha Ufundi Veta, kilichoko Mkoani Morogoro.

  • MSD Kilimanjaro Yajadili Mbinu Kuboresha Uhusiano na Huduma kwa Wateja

    ARUSHA.

    MSD Kanda ya Kilimanjaro imekutana na wateja wake wanaopata huduma kutoka Kanda hiyo ambao ni kutoka mikoa yaArusha, Kilimanjaro na Manyara, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanagusa pande hizo, kwa lengo la kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi. 

    Mkutano huo wa siku moja umefanyika Mkoani Arusha ukiwa na lengo la kujenga uhusiano mzuri baina ya MSD Kanda ya Kilimanjaro na wateja wake wote wanaohudumiwa na Kanda hiyo.

  • MSD Kanda ya Mbeya, Yateta na Wafamasia Kuboresha Huduma

    MBEYA:

    MSD Kanda ya Mbeya imefanya kikao na wafamasia kutoka halimshauri 17 na wafamasia wa mikoa yote inayohudumiwa na Kanda hiyo

    Kwa upande wake Meneja wa MSD Kanda ya Mbeya Bw. Marco Masala amesema lengo la kikao hicho ni kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha huduma za upatikanaji wa bidhaa za afya katika mikoa hiyo, pamoja na kuimarisha uhusiano.

    Pamoja na mambo mengine kupitia kikao hicho wamekubaliana kuunda kamati maalum ya kudumu itakayosaidiana na Kanda ya MSD Mbeya kufuatilia utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye kikao hicho. 

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.