Skip to main content

MSD Kuimarisha Upatikanaji wa  Bidhaa za Maabara Nchini.

Bohari ya Dawa (MSD) imeadhimia kuboresha hali ya upatikanaji wa bidhaa za maabara nchini, ili kuimarisha uchunguzi wa vimelea vya magonjwa mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya (MSD) Rosemary Silaa, wakati alipotembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa - Bukoba na hospitali ya Wilaya ya Bukoba vijijini, ziara iliyolenga kupokea mrejesho wa huduma za MSD kutoka kwa wateja, ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 30 toka MSD kuanza kazi zake rasmi.

Silaa amesema MSD imechukua hatua mbalimbali za kuboresha eneo la maabara ikiwemo kuajiri wataalam wa kada hiyo, ambao kwa sasa wanapatikana Kanda zote za MSD.

Aidha, ameipongeza Serikali kwa juhudi za kufanya standardization ya mashine za maabara kuanzia ngazi ya zahanati hadi ngazi ya taifa, hivyo limebaki jukumu la MSD kuhakikisha vinapatikana kwa wakati na wakati wote, mchakato ambao unaendelea hivi sasa. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa Bukoba Dkt. Sophia Mosha amesema huduma za maabara zimekuwa muhimu katika upimaji wa sampuli inapotokea magonjwa ya mlipuko, hivyo kuiomba MSD kuimarisha eneo hilo, kama ilivyofanya kwenye maeneo mengine.

Aidha wameipongeza MSD kwa kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya, kwani hivi sasa out of stock zimepungua na kiwango cha upatikanaji wabidhaa kimekuwa kikiongezeka siku hadi siku 

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Dkt. Gavyole Bandioti amepongeza mahusiano mazuri yalipo baina yao na MSD, huku akibainisha kwamba ukaribu huo umewawezesha kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili kwa wakati 

Kwa upande wake Meneja wa MSD Kanda ya Kagera, Kalendero Msatu, ameahidi kuendelea kushirikiana na wateja kwa ukaribu Ili kutatua changamoto zinazo wakabili wakabili Ili wateja wake.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.