Skip to main content

Wateja wa MSD Kanda ya Tanga Wapongeza Maboresho ya Huduma za MSD

Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga wameipongeza MSD kwa maboresho makubwa inayoendelea kuyafanya ya usambazaji wa bidhaa za afya kwa wakati.

Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD ambaye pia ni Mlezi wa MSD  kanda hiyo, Dkt. Rukia Mwifunyi anayoifanya mkoani humo, kuzungumza na wateja wanaowahudumia ili kupata maoni yao juu ya huduma za MSD na kupokea changamoto zao ili ziweze kufanyiwa kazi.

Ziara hiyo inafanyika ikiwa ni moja ya matukio ya kuadhimisha miaka 30 ya utendaji wa MSD tangu 1994,ambapo kabla ya hapo ilikuwa ikiitwa Central Medical Store (CMS)

Mfamasia wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga (Bombo), Kibwana Mgude alipongeza MSD kwa kuwafikishia bidhaa za afya kwa wakati na kueleza kuwa sasa upatikanaji wa bidhaa za afya umeboreshwa kwa kiwango cha juu.

“ Sasa hivi tunapokea dawa na vifaa tiba kwa wakati tunakila sababu ya kupongeza maboresho haya ya MSD,” alisema Mgude.

Kwa upande wake Magdalena Chambo ambaye ni Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Nkumba alisema utaratibu unaofanywa na MSD wa kuwapelekea bidhaa za afya hadi vituoni mara sita (6) kwa mwaka ni mzuri.

Dkt. Mwifunyi akizungumza wakati wa ziara hiyo alipongeza MSD kwa kazi kubwa wanayoifanya ambapo alitumia nafasi hiyo kuomba kudumisha ushirikiano baina yao na wateja wao wanaowahudumia.Aliwasisitiza wateja hao wa MSD kutoa mapendekezo yao ambayo wataona yana tija kwa ajili ya kuboresha shughuli zinazofanywa na MSD.

“ Utoaji wa huduma bora za usambaji wa vifaa tiba na dawa ni jambo jema kwani jamii na taifa wanatutegemea,” alisema Dkt. Mwifunyi.

Katika ziara hiyo Dkt. Mwifunyi aliongozana na baadhi ya maafisa wa MSD kutoka Kanda ya Tanga na Makao Makuu wakiongozwa na Meneja Huduma za Sheria MSD, Elisamehe Macha, MenejaMawasiliano naUhusiano wa MSD Bi. Etty Kusiluka na Meneja Huduma kwa Wateja Dkt. Pamella Sawa.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.