Skip to main content

Uzalishaji wa Bidhaa za Afya

Katika kuongeza ufanisi wa usimamizi wa shughuli za uzalishaji na kuhakikisha utekelezaji wa miradi kwa wakati, MSD imeanzisha Kampuni Tanzu inayoitwa “MSD Medipharm Manufacturing Company Limited” ambayo inajukumu la kusimamia shughuli za uzalishaji wa bidhaa za afya na itakuwa na uwezo wa kuingia ubia na wawekezaji wengine. Kwa sasa kampuni hii inasimamia viwanda vya Barakoa (Surgical na N95 Mask) Dar es salaam na kiwanda cha Mipira ya Mikono Idofi Makambako, Mkoani Njombe. Viwanda vya kuzalisha barakoa na mipira ya mikono vimekidhi viwango vya ubora wa kuzalisha bidhaa hizo na hivyo kutunukiwa ithibati ya ubora “Good Manufacturing Practice” (GMP) inayotolewa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).

Kiwanda cha mipira ya mikono kina uwezo wa kuzalisha mipira ya mikono 20,000 kwa saa ambayo ni sawa na jozi 10,000 kwa saa. Kiwanda cha barakoa kimefanikiwa kuzalisha na kusambaza barakoa zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni nne (4) na kufanya nchi kujitosheleza kwa uzalishaji wa barakoa. Katika hatua nyingine MSD inamiliki eneo katika kijiji cha Ng’hami kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha bidhaa za afya zitokanazo na malighafi ya pamba kama mashuka, gozi, bandeji, na pamba za hospitalini.

Eneo hili lipo katika Halmashauri ya Maswa, Mkoa wa Simiyu na lina ukubwa wa hekari 102 lenye namba ya usajili 5459.   Lengo kuu ni kupunguza uagizaji wa bidhaa hizi kutoka nje ya nchi ambapo kiasi cha shilingi bilioni 26 hutumika katika kununua bidhaa hizo kwa mwaka.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.