Mkurugenzi Mkuu MSD, Awafunda Wataalamu Sekta ya Afya
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Saul Mhidze amesema kuwa na wataalam wa ndani wanaomudu kutumia vifaa vya maabara na kuvikarabati wenyewe ni hatua nzuri itakayopunguza gharama. Ameyasema hayo alipozungumza na Wataalamu wa maabara, Mafundi Sanifu na Wahandisi vifaa tiba kutoka MSD,Halmashauri na Hospitali mbalimbali nchini, ambao wapo kwenye mafunzo ya namna ya kufunga, kutumia na kuzifanyia matengenezo mashine mbalimbali za maabara ambazo zinatarajiwa kufungwa nchi nzima. Mashine hizo za maabara zitapunguza gharama za vipimo vya uchunguzi wa magonjwa kwa zaidi ya asilimia hamsini.