Skip to main content
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makorora mkoani Tanga, Dkt.Angelina Meshack, Akiongea na Waandishi na Ujumbe Maalum Kutoka MSD (Hawapo Pichani) Walipomtembelea Ofisini Kwake, Kupata Mrejesho wa Huduma Zitolewazo na Bohari ya Dawa (MSD)

MSD Yapongezwa kwa Mageuzi ya Huduma, ndani ya Muda Mfupi.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makorora mkoani Tanga, Dkt.Angelina Meshack ameipongeza serikali kupitia MSD, baada ya kupokea vifaa vya chumba cha upasuaji ikiwemo kitanda cha upasuaji, mashine ya dawa ya usingizi na taa zinazotumika wakati wa upasuaji, amesema vifaa hivyo ni msaada mkubwa katika kituo hicho kwani awali kulikuwa na changamoto kwenye hutoaji huduma.

"Awali tulikuwa hatufanyi upasuaji kabisa kwa hiyo tulivyopokea fedha kwa ajili ya ukarabati majengo ya kufanyia upasuaji tulifanya hivyo na baadae vifaa vililetwa na MSD na kuanza kutoa huduma za upasuaji". Amesema Dkt.Angelina

 Amesema baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo walianza kutoa huduma ya upasuaji mbalimbali wa mama wajawazito pamoja na upasuaji mdogo kwani hapo awali walikuwa wanawapeleka wagonjwa hospitali ya Bombo kwa sababu huduma hiyo haikuwepo hapo kituoni.

"Kwa ujio wa vifaa hivi imerahisisha mama mjamzito akipata changamoto moja kwa moja tunaweza kumpa huduma ya upasuaji na tunaokoa maisha ya mama pamoja na kichanga". Amesema.

 Pamoja na hayo Dkt.Angelina amesema walikabidhiwa pia na jenereta kwa ajili ya hospitali hiyo lakini wakaamua kuwasiliana na ofisi ya mganga mkuu ili waweze kuichukua na kuikabidhi kwenye vituo vingine ambavyo havina jenerata kwa sababu kituo hicho kilikuwa na jenerata ambayo walikuwa wameshanunua awali.

 Ameeleza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa katika kituo hicho ni nzuri kwani kwa sasa dawa muhimu zinapatikana kwa asilimia 90 na wanaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.