Skip to main content
Kamati ya Bunge ya Afya, Maendeleo na Huduma za Jamii ya Bunge la Zambia Ikiwa kwenye Ziara ya Kutembelea Viwanda vya MSD.

Kamati ya Afya Bunge la Zambia, Yaipongeza MSD kwa Maboresho ya Utendaji na Ujenzi wa Viwanda

Kamati ya Bunge ya Afya, Maendeleo na Huduma za Jamii,ya Bunge la Zambia wamevutiwa na hatua ya Bohari ya dawa (MSD) kuanza kuzalisha baadhi ya bidhaa za afya kwa kutumia wataalam wake wa ndani.

Hayo yamebainishwa hii leo, tarehe 26/5/2022 baada ya Kamati hiyo ya Afya kutoka Zambia, kuitembelea MSD kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala yanayohusu mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya.

Akizungumza kwaniaba ya ujumbe huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge ya Afya, Maendeleo na Huduma za Jamii, ya Bunge la Zambia, Mhe.Dkt. Christopher K. Kalila amesema wamevutiwa na hatua ya Bohari ya dawa (MSD) kuanza kuzalisha baadhi ya bidhaa za afya kwa kutumia wataalam wake wa ndani.

 Mhe.Dkt. Kalila ameongeza kuwa MSD Tanzania ni kama pacha wa Bohari ya Dawa ya nchini Zambia, kwani sheria yao pia imefanyiwa mabadiliko na kuiwezesha Bohari hiyo kuanza kuzalisha bidhaa za afya.

 "Ni vyema taasisi zetu hizi mbili zikawa karibu ili kubadilishana uzoefu, na utaalamu katika maeneo mabalimbali ili kusukuma kwa pamoja ajenda ya uanzishaji wa viwanda

vya bidhaa za afya na kuondoa utegemezi wa bidhaa kutoka nje sambamba na kupunguza gharama." Alisema Dkt. Kalila.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.