Bohari ya Dawa Msumbiji Yapongeza Juhudi za MSD Kuboresha Huduma, Pamoja na Ujenzi wa Viwanda
Ujumbe kutoka Bohari ya dawa (CMAM) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (ANARME) Msumbiji leo wametembelea MSD Makao Makuu kwa lengo la kujifunza na kubadirishana uzoefu.
Ujumbe huo Msumbiji ulifanya ziara ya kutembelea maghala ya kuhifadhia bidhaaza afya ya MSD pamoja na kiwanda cha kuzalisha barakoa na kiwanda cha kuzalisha vidonge KPI.
Ujumbe huo umevutiwa na hatua ya MSD kuongeza jukumu la kuzalisha bidhaa za afya ambazo zinasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza Gharama za kuagiza bidhaa hizo kutoka nje.
Aidha, pamoja na mambo mengine ujumbe huo ulikutana na Kurugenzi za Ugavi na TEHAMA na kupata maelezo namna mifumo mbalimbali inavyofanya kazi katika mnyororo wa ugavi na kuahidi kuiga mazuri punde tu warejeapo nchini kwao.
Katika hatua nyingine ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea wateja wa MSD ambao ni hospitali ya Mifupa, MOI na Taasisi ya Moyo (JKCI) kwa lengo la kujifunza namna taasisi hizo zinavyoendesha shughuli zake.
- Log in to post comments